UNIONI YA KASKAZINI MWA TANZANIA
CHAMA CHA WACHUNGAJI/HUDUMA ZA MAOMBI
SIKU 100 ZA MAOMBI:
MACHI 27 – JULAI 2, 2020
“Kumlilia Yesu wakati wa Uhitaji wetu mkuu!”
Masomo haya yameandaliwa na Mark Finley ambaye ni msaidizi wa Halmashauri Kuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato
Yametafsiriwa na Moseti Chacha na kuratibiwa na Huduma za Maombi NTUC.
Juma la nane – Siku 100 za Maombi - May 15 – May 21, 2020
Kubadilishwa na Upendo wa Mungu
Derek Morris“Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, Ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.” – Yeremia 31:3
Mary Ann Roberts alikulia katika nyumba ya Kikristo, lakini akiwa mdogo hakuwahi kujikabidhi kwa Yesu kama Bwana na Mwokozi wake. Baada ya kumaliza chuo aliolewa, na mume wake akajiunga na jeshi, kisha wakahamia Ulaya. Hapa ndipo Mary Ann alipokata mahusiano ya kanisa na kuanza kujirusha katika starehe.
Mwaka 1983 maisha yake yaligota. Akiwa katika ulevi uliodumu muda mrefu kati kati ya juma katika ile hali ya ulevi mzito aliugua kiasi kwamba hakuweza kuhudhuria katika kutaniko la kifamilia. Ndipo alipoamua kumwomba Mungu arudi katika maisha yake. Katika hali hiyo ya kushuka, taswira iliyokuja katika fikra zake ni baba mwenye upendo akimkimbilia “Mwana Mpotevu” ili kukutana naye na kumpokea. Mary Ann alijua fika kwamba yeye ndiye aliyekuwa huyo “Mwana Mpotevu.”
Alipotambua kwamba alihitaji kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yake, alimwandikia mchungaji wa Kikristo na kumweleza kwamba amejitoa kuwa mfuasi wa Yesu. Mke wa mchungaji huyo alielewa ugumu wa kubadilika kwa Mary Ann, hivyo akaamua kumtegemeza kwa kumpigia simu na kuomba naye kila siku asubuhi kwa kipindi cha mwaka mzima.
Pamoja na kwamba Mary Ann alikuwa akihudhuria kanisani, na Mungu alionekana
kuwa sehemu muhumu ya maisha yake, bado alihisi kwamba kuna kitu kilikuwa
kinapungua – kwamba Mungu alikuwa na jambo muhimu kwa ajili yake ambalo alikuwa
hajaligundua. Siku zote alitamani kwamba angeendeleza elimu yake, hivyo akaamua
kurudi chuoni na kuendelea na shule. Pengine kufanya hivyo kungejaza ombwe
lililokuwa ndani ya moyo wake. Alituma maombi kusomea shahada ya uzamili katika
sayansi, akakubaliwa na kusajiliwa, hatimaye akamaliza pia ngazi ya uzamivu katika
sanyansi ya neva. Lakini bado maisha yake yalionekana kama hayajakamilika.
Mwaka 2001 katika kipindi cha kipupwe, Mary Ann alihudhuria makambi kule Carolina
ya kaskazini. Kwa sehemu kubwa alivutiwa kujichanganya na marafiki, hivyo alipendelea kukaa sehemu ya nyuma kwenye ukumbi wa mikutano. Katika moja ya mikutano alimsikia Mwinjilisti wa Kikristo akiwakaribisha wale wenye shauku ya kushiriki katika mradi wa huduma kule Kenya wajitokeze ka kukutana naye baada ya huduma.
kumtumia katika mavuno yake.
Je, utamruhusu Mungu akutumie katika mavuno yake? Inawezekana hali isiwe kama ilivyokuwa miezi mitatu iliyopita kabla janga hili halijafikia upeo. Laini bado kuna mengi ya kufanya, na kuna roho nyingi zinasubiri kusikia Habari Njema! Mwombe Mungu na kumuuliza kile ambacho angependa ufanye.
Derek Morris ni mwenyekiti wa Hope Channel International. Kwa maandiko ya hamasa kama haya, tunakushauri usome kitabu chetu cha wiki kilichoandikwa na Derek Morris chenye kichwa kisemacho “The Radical Prayer” ambacho kimetumika kuleta haya masomo ya juma hili.”
Maswali kwa Undani wa Moyo: Je, kuhusu maisha yetu leo? Tumemruhusu Mungu atutumie katika mavuno yake? Ikiwa tunahisi kuwa tumetanga mbali kutoka kwake, tukumbuke kwamba anasubiri akinyoosha mikono ya upendo kuashiria kwamba turudi kwake. Siyo tu kwamba anataka kutukaribisha nyumbani, bali pia ana sehemu maalum aliyotutayarishia kuhudumu kila mmoja wetu. Je, tutafungua mioyo yetu kwa wito wake?
Changamoto ya Moyo iliyo hai: Hebu jaribu kuchunguza njia mbalimbali ambazo Mungu anatumia kuonesha upendo wake kwetu. Pengine utauona upendo wake kupitia kwa wengine, kupitia katika maumbile ya asili, au kwa namna nyingine tofauti.
“Mungu anatupenda, siyo kwa sababu ya upataniso mkuu, bali alitupatanisha kwa sababu anatupenda upeo. Mungu aliweza kumwaga upendo wake kwa ulimwengu uliopotea kupitia kwa Kristo. Tunasoma kuwa, ‘Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.’ 2 Wakorintho 5:19 Upendo kama huo hauna mfano. Watoto wa Mfalme wa mbinguni! Ahadi za thamani! Mada stahiki kwa ajli ya tafakuri! Upendo wa Mungu usio na mfano kwa ulimwengu ambao haukumpenda.” Steps to Christ, uk. 13, 15
Kuingia kwa undani – Mapendekezo ya Masomo ya ziada kwa Juma hili.
- Ellen G. White, Steps to Christ, sura ya 1, “God’s Love for Man.”
- Derek J. Morris, The Radical Prayer.
- Elizabeth W.: “Ninamsifu Mungu kwa nguvu zake za Uponyaji!”
- Washiriki kule Uingerza: “Msifu Mungu kwa kusikia maombi yetu na kutupatia chakula na fedha kwa namna ya miujuza wakati stahiki. Pia kwa kuponya tatizo langu la mgongo!”
- Wanasayansi wanafanya kazi kwa shauku kubwa ili wapate chanjo na tiba itakayosaidia kupunguza virusi vya corona. Kuna maendeleo makubwa yamefanyika na kuna matumaini!
2. Omba kwamba uinjilisti wote unaofanyika kwenye mitandao na katika shughuli za kanisa za kidijitali ziwe na mafanikio na kubarikiwa sana.
3. Waombee vijana walio katika bonde la kukata shauri kumfuata Kristo au kutokumfuata. Omba kwamba wapate uzoefu wa upendo na ukweli wa Yesu na wawe tayari kumtumikia maisha yao yote.
4. Ombea vikundi vingi vya makanisa ulimwenguni kote ambavyo havina majengo ya kukutania na wanatafuta maeneo ya kujenga. Omba pia kwamba Mungu awaamshe washiriki waingie katika shughuli za kuanzisha makanisa.
Siku ya 51 – Kitovu cha Maombi – Jumamosi, 16 May 2020
Kujitoa Kikamilifu kwa Mungu
“Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” – Warumi 5:8
“Mara tu dhambi ilipojitokeza, kulikuwa na Mwokozi. Kristo alifahamu kwamba angepitia mateso yote hayo, lakini alikubali kuwa m-badala wa mwanadamu. Mara tu Adam alipoanguka dhambini, Mwana wa Mungu alijitoa kama mdhamini wa ubinadamu.” In Heavenly Places, uk. 13.2
Maswali kwa Undani wa Moyo: Adam na Hawa walipotenda dhambi, ni Mungu ndiye aliyechukua hatua ya kwanza kuelekea kwa ubinadamu bila kujali kwamba amekataliwa na kutendewa dhambi. Alikuja na mtazamo wa neema, msamaha na ahadi, kwamba Yesu atamponda nyoka ambaye ni Shetani (Mwanzo 3:15) na akuwa kafara kwa ajli ya wokovu wao. Kristo bado anatembea akikuelekea wewe akiwa na mtazamo ule ule. Amejitoa kwako na kwa ajili ya wokovu wako. Je, utakimbilia kwenye mikono yake yenye upendo leo na kuikubali damu yake itakasayo na haki yake?
TAARIFA ZA SIFA:
- Kupona kwa Daktari Hammel (ambaye ni Daktari wa tiba katika Berrien Springs) kutoka katika ugonjwa wa virusi vya corona baada ya kuombewa na jumuia ya imani.”
- Kanisa kule China linastawi pamoja na makatazo kwa sababu ya ugonjwa wa virusi vya corona pamoja na ukomunisti. Mamia ya maelfu wanaunganishwa katika ibada ya mtandao.
2. Ombea viongozi na washiriki wa kanisa kule Indonesia ambapo wengine wamepata maambukizi ya virusi vya Corona na hata kufariki.
3. Ombea nchi ya Papua New Guinea kwa kuwa bado haijajizatiti kukabiliana na mfumuko wa ugonjwa huu wa virusi vya corona.
Siku ya 52 – Kitovu cha Maombi – Jumapili, 17 May 2020
Kujitoa Kikamilifu kwa Yesu
“Haruni akawaambia maneno yote Bwana aliyonena na Musa akazifanya zile ishara mbele ya watu. Watu wakaamini, na waliposikia ya kuwa Bwana amewajilia wana wa Israeli, na ya kuwa ameyaona mateso yao, wakainama vichwa vyao wakasujudu.”Kutoka 4:30-31
“Unatamani kujitoa kwake, lakini unajikuta mdhaifu kimaadili, unajikuta katika utumwa wa mashaka bado ukitawaliwa na tabia za maisha yako ya dhambi. Ahadi zako na maazimio yako ni sawa na kamba ya mchanga. Hauwezi kutawala fikra zako, mihemuko yako, na mivuto yako. Uelewa wa ahadi ambazo haukuzitimiza na maagano uliyovunja, Imani yako katika udhati wako inapungua na kukusababisha kudhani kwamba Mungu hawezi kukukubali; hauhitaji kukata tamaa. Unachotakiwa kutambua ni nguvu ya kweli ya dhamiri. Hii ndiyo nguvu inayotawala asili ya mwanadamu, nguvu ya maamuzi, au nguvu ya chaguzi. Kila kitu kinategemea utendaji ulio sahihi wa dhamiri. Mungu amempa mwanadamu nguvu ya uchaguzi, na ni ya kwake kabisa anatakiwa kuitumia. Hauwezi kubadilisha moyo wako, hauwezi kumpatia Mungu mivuto yako wewe mwenyewe; lakini unaweza kuchagua kumtumikia. Unaweza kumpatia dhamiri yako; na Yeye atafanya kazi ndani yako kule kutaka na kutenda kulingana na mapenzi yake. Kwa hiyo asili yako yote itatawaliwa na Roho wa Kristo; mivuto yako itaelekezwa kwake, mawazo yako yatakuwa na upatanifu naye.” Steps to Christ, uk. 47,
Maswali kwa Undani wa Moyo: Wana wa Israeli walipokabiliwa na uhalisia wa ahadi ya upendo wa Mungu ya ukombozi kutoka utumwani, mwitikio wao ulikuwa ni kujikabidhi, kujitoa kikamilifu na kuabudu. Kadiri unavyotafakari upendo huu wa Mungu usiopimika, utachagua kuitikia kwa mtazamo huohuo? Je, utampatia dhamiri yako, maisha yako, na moyo wako? Mungu ni mwema. Ana nia ya kusaidia na kuponya. Mchakato huo unaweza kuwa na maumivu makubwa, lakini ni mchakato
stahiki. Kwa nini usiachie dunia na kujitoa ukikabidhi kikamilifu maisha yako na nia yako kwa Mungu leo kwa kumwabudu?
TAARIFA ZA SIFA:
- Zuio kwa sababu ya virusi vya corona limesababisha ongezeko la shauku kwa injili kule Mashariki ya Kati. Watu mbalimbali wakikusudia wasifahamike wamejiunganisha kimtandao na makanisa.
- Harakati za maombi zinafanyika kwa wingi katika Divisheni ya Marekani ya Kati.
2. Waombee washiriki walio waaminifu ambao wanatumika katika hifadhi za vyakula wakati huu. Omba kwamba walindwe kutoka katika maambukizi kadiri wanavyohudumu kwa upendo katika jumuiya zao.
3. Waombee walei, wafanyakazi wa Biblia, na wainjilisti ambao wanategemea kilimo na shughuli zingine za kujitegemeza wao na familia zao. Omba kwa ajili ya wale wanaoishi na kutumika katika majimbo yaliyokumbwa na hali mbaya ya ukame.
Siku ya 53 – Kitovu cha Maombi – Jumatatu, 18 May 2020
Kujitoa Kikamilifu kwa Marafiki
“Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; Lakini yuko rafiki
aambatanaye na mtu kuliko ndugu.” Mithali 18:24
“Yonathani pamoja na kufahamu kwamba alizaliwa ili awe mrithi wa kiti cha enzi, bado kwa tamko la kimbingu aliachia nafasi hiyo kwa rafiki yake Daudi aliyekuwa rafiki, mpole wa moyo, na mwaminifu, akilinda maisha ya Daudi katika hatari ya maisha yake mwenyewe… Jina la Yonathani lina thamani mbinguni, na linasimama duniani kama ushuhuda wa kuwapo kwa nguvu ya upendo isiyokuwa na ubinafsi.” Education, uk. 157
Maswali kwa Undani wa Moyo: Urafiki wa Daudi na Yonathani ulikuwa na sifa za kiroho kwa kina ambazo zinaonekana kwa nadra sana sehemu nyingine yoyote. Urafiki wao ulijengeka katika agano takatifu la mapatano ya kutegemezana kiroho na kujitoa kikamilifu. Je, unaye rafiki wa kiroho? Wewe ni rafiki wa kiroho wa mtu fulani? Kwa nini usichague kujitoa kikamilifu kwa ukuaji wa kiroho wa rafiki zako ukiweka pembeni haja zako, starehe zako na kutenga wakati wako na upendo wako kuwategemeza marafiki na kutembea na Kristo?
TAARIFA ZA SIFA:Mikutano ya uinjilisti ya kimtandao ya “ItIsWritten” inatupatia taarifa za matokeo ya kushangaza kwa maelfu ya watu kushiriki na wengi wao kufanya maamuzi kwa ajili ya Kristo. Watafutaji wanaunganishwa na makanisa ya Waadventista wa Sabato mahalia kwa ajili ya kuwafuatilia.
- Wengi wa wale waliokuwa washiriki wa kanisa la Waadventista wa Sabato wanarudi kuunganishwa tena na kanisa, shukurani kubwa kwa kuongezeka kwa shughuli za kuwafikia katika mitandao.
2. Omba kwa ajili ya mikutano ya kiinjilisti iliyopangwa katika bonde la ufa kule Kenya ambayo inafanyika katika maeneo mapya ya himaya ya kanisa letu.
3. Omba kwa ajili ya kituo cha jumuia ya kanisa la Waadventista wa Sabato wa Phoenix Beacon Light kadiri washiriki wapya wanavyojitayarisha kuhudumia
jumuia yao
.
Siku ya 54 – Kitovu cha Maombi – Jumanne, 19 May 2020
Kujitoa Kikamilifu kwa Mwenzi/Familia yako
“Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake. Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.” Waefeso 5:22, 25; 6:1, 4 18:24
“Sababu ya mgawanyiko na kutokuelewana katika familia na hata kanisani, ni kujitenga kutoka kwa Kristo. Kumsogelea Kristo ni kumsogelea mwenzi wako. Siri ya umoja wa kweli kanisani na hata katika familia siyo diplomasia, au utawala, wala siyo jitihada za nguvu zisizo za kawaida katika kutafuta kushinda magumu – ingawaje hayo yatahitajika kutendeka – bali ni umoja na Kristo.” The Adventist Home, uk. 179
Maswali kwa Undani wa Moyo: Mwenzi wako pamoja na familia, ni watu katika maisha yako unaowajibika kwao; Kuwapenda, kuwategemeza na kuwanidhamisha kwa furaha, upendo, na kuwaleta katika uhusiano na Yesu. Je, utajitoa kikamilifu leo hii kueneza neema kama hiyo, msamaha na upendo ambao Yesu amekuonesha katika maisha yako na mwenzi wako pamoja na familia yako? Je, ni haja yako kuwa kiongozi wa kiroho katika nyumba yako? Mwombe Yesu leo upate kutembea naye kwa kina na kuunganika naye ili upate kumuakisi kwa mwenzi wako na kwa familia yako.
TAARIFA ZA SIFA:
- Prosper O: “Naam! Bila kujali ugonjwa huu wa virusi vya Corona, mimi nitaendelea kumwimbia na kumsifu Bwana aliye Juu.”
- Jon W: “Zahama hii imenipatia hitaji jipya la kuwa karibu na kutembea karibu na Kristo.”
2. Ombea siku ya tarehe 6 June ambayo siku ya “Maombi kwa Ndoa na Familia” iliyopangwa na Idara ya Huduma za Familia ya Halmashauri Kuu ya kanisa la Waadventista wa Sabato. (family.adventist.org)
3. Ombea watu wasiokuwa na wenza ambao wanajisikia upweke wakati huu. Omba kwamba wapate kuona mibaraka ya kuwa pekee kama matokeo ya kumtumikia Mungu. Omba kwamba ikiwa ni mapenzi ya Mungu, basi wapate wanza wanaomcha Mungu.
4. Ombea watu wanaohangaika na uraibu.
5. Ombea mshirki kule Trinidad ambaye binti yake aliuwawa miaka miwili iliyopita, na kijana wake ameuwawa mwezi wa tatu uliopita. Omba kwamba afarijiwe na pia apate ulinzi dhidi ya familia nyingine yote.
Siku ya 55 – Kitovu cha Maombi – Jumatano, 20 May 2020
Kujitoa Kikamilifu kwa Kanisa lako Mahalia
“Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika.” Matendo 4:32
“Waongofu wa Injili walikuwa ‘na moyo mmoja na roho moja.’ Shauku ya pamoja iliwatawala – mafanikio ya utume waliokabidhiwa; na kwamba kijicho hakikuwa na nafasi katika maisha yao. Upendo wao kwa ndugu zao na njia waliyokuwa wameichagua ilikuwa kubwa kuliko upendo wao kwa fedha na mali. Kazi zao zilishuhudia kwamba walihesabu roho za watu kuwa na thamani kuliko mali ya dunia hii.” Acts of Apostles, uk. 70
Maswali kwa Undani wa Moyo: Kuna wakati tunaweza kuvunjwa moyo na kanisa mahalia, au hata kanisa la ulimwengu. Hata hivyo lazima tufahamu kwamba kanisa ndilo bibi harusi wa Kristo. Kama vile Yesu alivyojitoa kikamilifu kwa kanisa lake, sisi tusingejitoa kwake pia? Wakristo wa awali walijazwa na Roho ya utayari wa kutoa kafara vyote kwa ajili ya utume na kanisa la Mungu. Kwa nini usimwombe Mungu leo hii akusamehe mwenendo wako wa dhambi ambao umewahi kuwa nao kwa bibi harusi wake, na kumwomba akubatize kwa Roho wake, na kukuwezesha kutafuta umoja, na
kusihi kwa kujikana nafsi ili kutegemeza na kubariki jumuia ya kanisa lako mahalia?
TAARIFA ZA SIFA:
- Tunamsifu Mungu kwa ajili ya makanisa mapya 900 yaliyoanzishwa kwa miaka michache iliyopita kwenye divisheni ya Amerika Kaskazini.
- Maombi ya mafunzo ya Biblia yameongezeka mara tano katika Divisheni ya Amerika Kusini tangu janga hili lilipoanza.
2. Omba kwa ajili ya mahitaji ya kanisa lako mahalia. Mahitaji ya kiroho na yale ya kimwili. Omba kwa ajili ya umoja, uponyaji, na kuhuishwa kwa kujitoa kikamilifu kwa ajili ya shughuli za kimisionari za kuwafikia watu.
3. Ombea wachungaji na viongozi wa kanisa wa union ya Haiti. Ombea makanisa katika baadhi ya majimbo ya Haiti ambayo yamejawa na makundi ya majambazi wenye silaha. Omba kwa ajili ya ustawi wa kiroho, kimwili, kifedha na kiakili kwa washiriki kule Haiti.
4. Omba kwa ajili ya washiriki ambao wameng’ang’ania mitazamo ya mafundisho yaliyopindishwa na kupotoshwa na wanajaribu kudanganya wengi.
5. Ombea washiriki wa zamani ambao wamejitenga kutoka katika kanisa na kuunda vikundi vyao wenyewe vya madhehebu. Omba kwamba waongozwe katika ukweli.
Siku ya 56 – Kitovu cha Maombi – Alhamisi, 21 May 2020
Kujitoa Kikamilifu kwa Utume wa Mungu
“Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili
nipate watu wengi zaidi… Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate
kuwaokoa watu.” 1 Wakorintho 9:10, 22
Maswali kwa Undani wa Moyo: Kazi ya Umisionari na uinjilisti, siyo Nyanja za huduma zilizotengwa kwa ajili ya wachungaji au wainjilisti waliopitia kwenye mafunzo pekee. Kila muumini ambaye moyo wa Yesu unadumu ndani yake kupitia kwa Roho, anaitwa kuangaza nuru katika dunia hii kupitia katika maneno ya ukweli na vitendo vya upendo.
Kwa nini usimwombe Kristo sasa hivi akuoneshe nani, na ni wapi ni eneo lako la utume leo hii? Sihi kwa ajili ya huruma ya dhati kwa roho zinazopotea na ujasiri wa kushiriki Imani na upendo kwa watu walio katika maeneo yako ya mvuto.
TAARIFA ZA SIFA:
- Familia ya Makoba: “Maombi ya siku 100 yamekuwa na uzoefu mzuri kwetu kama familia. Ingawaje hali inayotuzunguka inaonekana kuwa ya kutisha, kama familia tunachukulia kipindi hiki kama wakati wa kurejesha maisha yetu kwa Yesu huku tukifuatilia hii program ya siku 100 za maombi kwa umakini.”
- Timu ya vijana ya “Utume wa Mwaka Mmoja” kule Guwahati nchini India, iliweza kuwafikia maelfu ya Wahindu wakiwa na ujumbe wa afya kabla tu ya kuibuka kwa ugonjwa huu wa virusi vya corona.
2. Ombea hospitali zote za Waadventista wa Sabato kwa namna walivyo na mahitaji mengi wakati huu za zahama ya ugonjwa wa corona. Omba kwamba madaktari na wauguzi wote wawezeshwe na Roho Mtakatifu wawe mashahidi kwa wagonjwa wao.
3. Ombea vituo vya kanisa vya ‘Life Hope’ maeneo yote ulimwenguni viwe ni nguzo za nuru wakati huu wa siku zenye giza.
4. Ombea majiji makubwa katika eneo lako kwamba Mungu atupatie namna ya kuwafikia watu katika maeneo hayo.
5. Omba kwa ajili ya wamisionari walio katika msitari wa mbele, hasa katika dirisha
la 10/40 ambao wanatafuta kumfikisha Yesu katika jumuia zao ambazo
zimetawaliwa na Shetani kwa maelfu ya miaka.
No comments:
Post a Comment