IBADA YA SABATO TAKATIFU 16/05/2020
MNENAJI MKUU:
Mwl. ELIHURUMA YESSAYA MMBAGA
Mwl. ELIHURUMA YESSAYA MMBAGA
FUNGU
KUU: ZEKARIA
9:11-12
WIMBO
MKUU (Nyimbo za kristo);
NO 119 Alilipa bei
KWAYA(WIMBO):HEBU NENDA HOSPITALINI
SOMO; KUIRUDIA NGOME.
Ø Ananukuhu kitabu cha Zekaria 9;11-12 (Irudieni
ngome enyi wafungwa wa tumaini)
Wito wa biblia katika dunia ya leo
ni kuirudia Ngome.
Je
ngome ni nini?
Ngome ni eneo/jengo kubwa lililoimarishwa kwa silaha za kivita kwa ajili ya
kujihami na maadui (Kamusi ya Kiswahili) .Hii ilifanyika saana nyakati za zamani, mfano
taifa la Israel na maadui zao tofauti na sasa. Ilisadikika ndipo penye usalama
pekee wakati wa vita.Miji mingi ilizungushiwa ngome kwa kutumia kuta zilizo
imara. Ilimpasa adui avunje kwanza ngome ya mji huo ndipo aweze
kuwafikia mateka wa eneo hilo na bila kuvunja ngome huwezi kufanikiwa katika
uvamizi huo na kupata mateka.
Mtunga ZABURI 27;1-2 anasema (Bwana
ni ngome yangu nimhofu nani?) anasema pia BWANA ni NGOME ya uzima.shetani hawezi kutuweka mateka
kama BWANA ndiye ngome yetu.
Kisa cha mtu mmoja aliyeiacha
ngome
Mtu huyu alikuwa katika ngome
akaiacha na baadaye akairudia ngome. Je wajua ni nani na ni kwa
vipi aliirudia ngome?.Ambatana nami
asubuhi ya leo.
Ø Ngome
kamwe haiwezi kukuacha bali wewe ndiye waweza kuiacha ngome.mfano, Mungu hawez kutuacha bali sisi ndio
twaweza kumuacha Mungu.
Kitabu cha Waamuzi 13;16 kinaeleza
ujio wa Samsoni mnadhiri wa MUNGU na uwepo wa wazazi wake. Wazazi wa Samson wanapewa
maelekezo namna ya kumlea mototo huyu (Samson).
Samson
alipoiacha ngome maadui walipata nafasi ya kumfanya yeye mateka.
Kejeli dhidi ya shujaa huyu wa
Mungu zilimfanya samsoni aonekane kuwa yeye si kitu kabisa.
Walifanikiwa kufungua mlango wa
ngome ya Samsoni kwa kutumia Delila(mke wa samsoni) kisha kumtoboa macho.
Upofu wa macho ya Samsoni ulimfanya afungue macho ya
kiroho hata akarudishiwa nguvu za kuwaangamiza wafiristi.
Ili
uweze kufumbuliwa macho ya kiroho kubali kutobolewa macho ya kimwili kwanza.
Samsoni
anafanikiwa kuirudia ngome.alipokuwa amekamatwa na
kuwekwa mbele ya wafiristi katika jengo la maonesho,kama mfanya maonesho. Samsoni alijihisi kama kiongozi mkuu wa wenye dhambi.
Nakupendekezea leo umpende (na kuwa kama) Samsoni aliyetobolewa macho na si Samsoni asiyetobolewa macho
Kwa
nini nakupendekezea samsoni aliye tobolewa macho?
Kwa sababu ya upofu wa macho yake samsoni anaanza kuwa;
·
Mnyenyekevu.
·
Mwenye maombi mengi.
·
Mwenye Kumtafuta Mungu.
·
Anajiona mwenye mapungufu makubwa sana.
·
Alimtafuta Mungu katika nyakati za
kujiliwa kwake.
Samsoni anatumika kama kiburudisho mbele ya miungu ya
wafilisti(dagon) na kelele za dhihaka za wafilisti kwa samsoni ziliibua hisia
za kumtafuta Mungu ndani ya moyo wake na shetani alitumia nafasi hii kupitia
wafilisti kwa kumzomea na kuonyesha kuwa yeye(Samsoni) si kitu. Lakini Samsoni
alisema moyoni mwake KRISTO ni vyote kwangu na akiwepo yeye ni salama rohoni.
Waamuzi 16;28 (Samsoni anamwita BWANA)Bwana niokoe kwa wakati huu tu..
Waamuzi 16;28 (Samsoni anamwita BWANA)Bwana niokoe kwa wakati huu tu..
Wakati mwingine tunazama dhambini na tunapohitaji kutubu
shetani anatukumbusha dhambi zetu na tunashindwa kumrudia Mungu wetu.Lakini kwa
Samsoni hakujali,Alimwita Bwana na kuomba nguvu yake kwa wakati mchache tuu.
Kama kwa samsoni, AMINI SASA UMESAMEHEWA usiogope Mrudie Mungu naye yuko tayari
kukupokea.
Wito
wangu kwako leo ni kwamba kila mtu na
airudie ngome (Zaburi 27;1)
Nitakapo simama miguuni pa Yesu taji nitaweka miguuni pake
MUNGU
AWABARIKI
Kutazama ibada hii bofya hapa pia usisahau ku'like na ku'subscribe katika YOUTUBE channel yetu ili uweze kupata updates mbalimbali na kubarikiwa.
Pia waweza kutazama video hii hapa chini
No comments:
Post a Comment