SOMO: USIKU UNAPOINGIA
MHUBIRI: Mwl. MKAMA DICKSON
FUNGU KUU: Kutoka
29:45-46
Mhubiri alianza na kisa alichopitia maishani mwake. Mnamo
mwaka 2019 akiwa jijini Dodoma
akifanya biashara zake miaka miwili baada ya kuoa, kwa bahati mbaya yeye na wenzeke kumi
walikamatwa na maofisa wa jeshi la polisi na kuwekwa rumande. Waliamriwa kutoa
kiasi cha Tsh. milioni moja kila mmoja ili kuachiwa huru ama kutumikia kifungo kisichopungua
miezi mitatu gerezani. Wakiwa rumande,
wenzake walifanya juhudi za kulipa faini hiyo ili waachiwe ila yeye hakufanya
jitihada hizo. Askari wale walimuuliza kwanini hafanyi harakati za kutoa kiasi
hicho, akajibu hana pesa hiyo, wakamwambia atabaki humo. Alijikabidhi mikonono
mwa Bwana Yesu kupitia maombi.
Ghafla! mke wake alianguka kwa mshituko wa moyo na kupoteza
fahamu kisha kupelekwa hospitali, ndipo
aliwaendea askari wale kuwaeleza namna ya kumsaidi ili ili aende
kumuuguza mkewe kwani hakuna ndugu wa karibu wa kumhudumia. Askari wale walimuuliza
kiasi cha pesa alichonacho ili wamuachie huru, akajibu kuwa ana kiasi cha Tsh
elfu 30 tu lakini kwa mashaka kwani nayo hakuwa nazo mfukoni(cash). Askari wale
walikataa kumkubalia lakini wakaenda
kujadili pembeni kisha wakamwita na kuweka mzigo wake kama dhamana kisha
wakamuachia.
Yohana 9:4
Yesu Kristo Anatukumbusha
kuwa kuna wakati wa kufanya kazi na upo
wakati tutapumzika kwani hatutaweza kufanya kazi hiyo. Yesu aliwaambia
wanafunzi wake juu ya kufanya kazi kwa
bidii kwani kuna wakati watakuwa wagonjwa ,katika umaskini,shida za
kifamilia,mfadhaiko au kufikia umri wa uzee ambapo watashindwa kufanya kazi
ipasavyo.
Katika kitabu cha Mhubiri, Suleiman anasema ukiwa kijana
unaweza kwenda popote pale na kwa mwendo wowote, lakini ukiwa mzee hutaweza
utapelekwa hata usikokutaka tena kwa mwendo usioutaka.Hivyo basi wakati tungali
na nguvu yafaa tumtegemee Mungu katika maisha yetu hasa wakati ambapo giza
linapoingia katika maisha yetu.
Tajiri mmoja katika mji Fulani aliyekuwa mfanyabiashara
maarufu katika mji ule,alikuwa na familia yake(mke wake na motto mmoja wa kike)Siku
moja asubuhi akiwa njiani kuelekea katika biashara zake akiwa katika gari lake
alipata ajali iliyotokana na tairi la mbele la gari yake kupasuka na gar
kupinduka.gari lake lilibondeka sana na raia walipo kuja kumsaidia baada ya
kumtoa akawa amevunjika mikono na miguu,hivyo wakampeleka hospitalin kwa
matibabu kasha akakaa kwa siku kadhaa akarudishwa nyumbani.baada ya siku chache
mke wake alipata mwaliko wa sherehe ya harusi ya mdogo wake baada ya kujadili
kama familia tajiri huyo alikubali mkewe aende kwa sherehe.Baada ya sherehe
kuisha walianza safari yeye na mwanae kurudi nyumban wakiwa njiani walikutana
na roli lililokuwa limepoteza mwelekeo kasha kugongana.Watu walipokuja kutoa
msaada walikuta mama huyo na binti yake wamepoteza maisha palepale,kumbe ni mke
wa Yule tajiri,n nani atapeleka taarifa kwa tajiri Yule kilema?kijana mmoja
akaamua kwenda,alipompa taarifa Yule tajiri aliinua macho yake juu kasha akasema
‘Bwana niko peke yangu kaa nami”
‘Kaa nami” ni
maneno yaliyotumiwa na Pr HENLY FRANCIS
aliyetunga wimbo no 91 katika nyimbo za
Kristo baada ya kukutana na changamoto katika maisha yake ikiwa ni pamoja na
ugonjwa na kukata tamaa, Aliita Bwana kaa nami. Bwana akikaa katika maisha yetu tutayashinda
yote yanayo tufedhehesha,.Mwite Bwana naye ataitika maana ameahidi.
MUNGU AWABARIKI NA
MUWE NA SABATO NJEMA.
God bless our families, use us the way you want to glorify your name.
ReplyDelete