BUSEGWE GIRLS' HIGH SCHOOL

Tunapokea wanafunzi Kidato cha kwanza hadi cha nne kuanzia tarehe 7/1/2021 Pia nafasi za wahamiaji kidato cha tano zipo!
Mawasiliano: 0759346439 au 0745114360
NYOTE MNAKARIBISHWA

SIKU 100 ZA MAOMBI: JUMA LA SABA

KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO
UNIONI YA KASKAZINI MWA TANZANIA
 
CHAMA CHA WACHUNGAJI / HUDUMA ZA MAOMBI
 
SIKU 100 ZA MAOMBI:
 
MACHI 27 – JULAI 2, 2020
 
“Kumlilia Yesu wakati wa Uhitaji wetu mkuu!”

Kitu Bora cha Kupata
 Masomo haya yameandaliwa na Mark Finley ambaye ni Msaidizi wa Halmashauri Kuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato
Yametafsiriwa na Moseti Chacha na kuratibiwa na Huduma za Maombi NTUC.



“Kumlilia Yesu wakati wa uhitaji wetu mkuu!”
 
Juma la Saba – Siku 100 za Maombi, May 8 – May 14, 2020
Kitu Bora cha Kupata
Na Ron Clouzet
 

Siku ya 43 – Kitovu cha Maombi – Ijumaa, 8 May 2020
 
Mwaka 2001 nilikaribia kupoteza uhai wangu. Daktari wa huduma za dharura alisema kwamba nilibakiza saa tatu nipoteze maisha. Nilishikwa na malaria nikiwa katika uinjilisti pamoja na wanafunzi wangu kule Afrika Magharibi, na dalili zilijitokeza siku kadhaa baada kurudi kwangu Marekani. Homa ilipanda, nikaishiwa maji mwilini,kichwa kikiniwanga sana. Nilijisikia mgonjwa hata nikadhani baada ya dakika chache nitapoteza fahamu na hatimaye kufa. Dalili hizo zilipojitokeza, nilikuwa katika shughuli za kawaida za kanisani. Niliondoka asubuhi kwenda uwanja wa ndege ili niwahi kurudi nikimwomba Mungu aniwezeshe kurudi nyumbani kwa shughuli ambazo zingefuata. Kama ningekufa, nilitamani itokee nikiwa nyumbani.

Mke wangu alinikimbiza hospitalini kwenye chumba cha wagonjwa mahututi. Nilpofika tu nilikuwa nimeanza kuona vitu kama njozi vile, sikuweza kujizuia kutapika. Nilizimia muda mfupi baada ya kuingizwa kwenye chumba cha mahututi. Nilipozinduka, nakumbuka kuona kama maisha yalikuwa na kasi ndogo sana. Kila dakika ilionekana kama ni saa nzima, na saa ilionekana kama siku nzima. Nakumbuka mke wangu anayeitwa Lisa akiwaleta watoto wetu watatu, wakati huo wakiwa na umri wa miaka 14, 12, na 10 nikiwaona wanalia kimya kimya. Nakumbuka wauguzi pamoja na waganga
wengine wakiniangalia kwa kusudi moja la kutaka kuona mgonjwa wa malaria anakuwaje, kwa sababu ugonjwa wa malaria ni nadra sana Marekani.


Ilikuwa dhahiri kwangu kwamba nilikuwa nakaribia kukata roho. Baadaye nilijifunza kwamba aina hii ya malaria ni kali kuliko aina zingine. Aina hii inakuua, hata ukipona hautaonesha dalili tena hadi utakapoambukizwa tena. Watu wengi walianza kuniombea, mke wangu na watoto wangu waliomba, wazazi wangu na wanafamilia wengine waliniombea. Wenzangu katika chuo cha ‘Southern Adventist University nilipokuwa nikifundisha waliniombea. Wanafunzi wangu waliniombea, rafiki zangu kutoka sehemu mbalimbali za dunia waliniombea. Wachungaji wasio na idadi kote katika nchi yetu
waliniombea. Kwa hesabu za haraka haraka nimekadiria kuwa watu karibu 2,000 walikuwa wakiniombea siku hizo


Lakini kurudia hali yangu halikuwa jambo rahisi. Dawa stahiki haikuwapo. Madaktari walio marafiki zangu walianza kuwashinikiza madaktari wa hiyo hospitali wafanye haraka kabla hatujachelewa. Hatimaye dawa aina ya kwinini ilipatikana maeneo yaAtlanta, na waliweza kuleta kiasi. Hii kwinini ni dawa ya zamani iliyokuwa ikitumika
kutibu malaria na aina zingine za magonjwa ya ajabu ajabu, lakini haitumiki kabisa sikuhizi. Ni dawa yenye sumu kali na inaweza kuwa na madhara makubwa. Lakini hii ndiyo itakayoondoa malaria mwilini. Niliwekewa kwinini saa arobaini na nane baada ya
kulazwa hospitalini, lakini haikuleta matokeo ya kimiujiza yaliyokuwa yakitarajiwa. Siku moja baadaye, ilikuwa ni Sabato, nilikuwa bado naumwa kama mwanzo tu.


Katika hali yangu ya kupambana, mimi pia niliomba. Lakini maombi yangu yalijawa shukurani kuliko kusihi. Nilikuwa nimeshakabidhi maisha yangu mikononi mwa Mungu, na nilikuwa tayari kusema kwaheri kama ungakuwa ni wakati wangu kufanya hivyo. Jambo moja tu lililokuwa linanisumbua ambalo niliombea, ilikuwa ni kumwacha mke wangu na watoto watatu wachanga, nikiwaacha hao watoto bila baba yao. Lakini kwa hilo pia nilijifariji kuwa lilikuwa mikononi mwa Mungu. Nilikuwa na Amani kwamba mambo yote yangekuwa salama.


Siku ya Sabato mchana baadhi ya wafanyakazi wenzangu katika chuo kikuu na mchungaji wa kanisa walikuja kunijulia hali. Walifanya huduma ya kunipaka mafuta na kuniombea tena, kulingana na Maandiko katika kitabu cha Yakobo 5:13-15. Usiku ule Lisa alikaa pembeni yangu usiku kucha. Kwa kweli alionekana kuingiwa na woga akidhani ndio mwisho wangu. Karibu saa kumi na moja alfajiri, muuguzi alikuja na kuchukua damu kidogo ya kipimo kama walivyofanya kila siku asubuhi. Kama saa nne baadaye, tabibu aliingia chumbani kwangu. Kwa mara ya kwanza niliweza kuinuka na kukaa. Akaniambia kwamba malaria imekwisha kwani wadudu hawaonekani tena kwenye damu yangu. Kwa namna fulani ilikuwa imeondoka. Alionesha mshangao kwamba ile dawa imefanya kazi vema na haraka kiasi hicho. Lakini nilijua wazi kwamba kulikuwa na sababu nyingine iliyofanya sasa sina malaria. Yalikuwa ni maombi ya wapendwa na watakatifu wa Bwana. Mungu kwa neema yake aliridhia kuniponya, ninaamini ni kwa sababu watu wake walimwomba afanye hivyo.

“Huyo huyo Mwokozi mwenye rehema yu hai leo, na yuko tayari kusikia maombi yanayotolewa kwa uaminifu kadiri anavyotembea kwa mwonekano kati ya watu… Ni sehemu ya mpango wa Mungu kwamba atupatie baada ya maombi ya Imani kile ambacho angeweza kutupatia bila sisi kuomba.” (
The Great Controversy, uk. 525). Yesu hakuhitaji kuniponya, sikuwa namdai kitu. Mimi nilikuwa nawiwa naye kila kitu, na bado nawiwa naye. Lakini bado alitenda.

Siyo kila hali inayotishia maisha yenye mwisho unaofanana. Lakini Mungu anayeponya
ni mmoja Yule, bila kujali hali. Anaweza kutumainiwa. Anaweza kupewa shukurani kwa
kila namna, kwa sababu hakuna namna anayoweza kujibu maombi yetu kwa kuumiza
nafsi zetu. Chochote tunachopokea kutoka kwake ni kile kilicho bora kwetu.


Ron E. M. Clouzet, DMin, ni Katibu wa Idara ya Huduma za Kichungaji wa Divisheni ya Kusini
mwa Asia ya Pacific. Yeye pia ni mwandisi wa kitabu cha “Adventist Greatest Need; The Outpouring of the Holy Spirit.”

 Maswali kwa Undani wa Moyo: Je, unaamini kwamba Mungu anaweza kuponya magonjwa ya kila aina, pamoja na ugonjwa unaombukiza wa dhambi? Je, umemlingana Mungu katika maisha yako leo? Je, una Amani na Mungu kila dakika inayopita?

Changamoto ya Moyo iliyo hai: Magonjwa ni sehemu ya dunia hii iliyovunjika. Hakuna mtu aliye salama dhidi ya magonjwa. Lakini tuna chaguzi zetu za namna tunavyoyakabili haya magonjwa. Tunaweza kumshikilia Yesu nyakati za uhitaji mkubwa, tukiomba uponyaji wa kimwili na wa kiroho, na tunaweza kuwa na uhakika kwamba lolote litakalotokea katika ugonjwa halitaondoa Amani yetu kwa sababu tunamtazama Yeye. Kuwa na Imani iliyo imara wakati wa ugonjwa kunaanza na kuwa
na Imani iliyo imara wakati wa uzima ukiwa na afya. Je, utachagua kumwamini leo?” Uko tayari kukubali hata kifo, ukielewa kwamba hatimaye magonjwa haya yote yataponywa katika asubuhi ile ya ufufuo kwa wale waaminio?


“Bwana wetu Yesu Kristo alikuja ulimwenguni humu kama mtumishi asiyechoka kwa mahitaji
ya muhimu ya mwanadamu. Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, alichukua magonjwa yetu
ili aweze kuhudumia kila hitaji la ubinadamu. Alikuja kuondoa mzigo wa ugonjwa na uharibifu
wa dhambi. Ilikuwa ni utume wake kuwarejesha wanadamu katika utimilifu; Alikuja kuwapatia
afya na Amani na tabia kamilifu.”
Ministry of Healing, uk. 17

Kuingia kwa undani Mapendekezo ya Masomo ya ziada kwa Juma hili.
  • Ellen G. White, Ministry of Healing, sura ya 16, “Prayer for the Sick.”
  • Ron Clouzet, Adventism’s Greatest Need: The Outpouring of the Holy Spirit.

Taarifa za Sifa!
  • Brittney na Vanessa B.: “Kanisa letu lilianza kukutana kwa mtandao kila siku usiku ili kuomba. Kufanya hivi kumemsogeza kila mmoja wetu kwa mwenzake kwa sababu tunaonana kila siku. Ni mbaraka mkubwa!”
  • Mico F.: “Hali hii imetusaidia kutambua kwamba kanisa siyo jengo, bali ni watu!”
MAMBO YA KUOMBEA1. Ombea makanisa ambayo yamepoteza washiriki wake kwa sababu ya ugonjwa huu wa virusi vya corona.
2. Ombea washiriki wanaopambana na masuala mbali mbali ya afya kama vile saratani, magonjwa ua ukosefu wa kinga za mwili, msongo, na mengine yote.
3. Ombea washiriki wa zamani wa kanisa la Waaventista wa Sabato ambao wamerudi nyuma na kuliacha kanisa. Omba kwa ajili ya watu katika maeneo yao ya kujidai, ambao wameongozwa mbali na Mungu kwa sababu ya mambo yaliyopo katika maeno yao ya kujidai.
4. Omba kwa jili ya washiriki wapya waliojiunga na kanisa la Waadventista waSabato kupitia njia mbalimbali za uinjilist wa kuwahusisha washiri (TMI) kwa miaka kadhaa iliyopita.
 


Siku ya 44 – Kitovu cha Maombi – Jumamosi, 9 May 2020 
Elimu ya Yesu
“Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.” – Yohana 17:3

“Yesu alikuja kumdhihirisha Mungu ulimwenguni kama Mungu wa Upendo, aliyejawa
rehema, upole, na huruma. Giza nene alilotumia Shetani kujaribu kufunika kiti ya enzi
cha Uungu limeondolewa mbali na Mkombozi, na Baba amewekwa bayana kabisa kwa
wanadamu kama nuru ya uzima.”
5T 738.4.

Maswali kwa Undani wa Moyo: Uzima wa milele hauhusu tu kuishi milele, bali uzima wa milele ni kuendelea kuzamisha uhusiano wako wa upendo na Mungu. Je, unafahamu kwa undani ukweli kumhusu Yesu, au unamfahamu kwa karibu, yeye kama Mwokozi na rafiki yako? Kwa nini usianze umilele leo kwa kumwomba Yesu ajidhihirishe kwa undani kwako, kadiri unavyotenga muda katika maombi, usomaji wa Biblia na kushiriki upendo wake na ukweli kwa wengine?

TAARIFA ZA SIFA:
  • Thierry T.: “Ninashiriki ‘Siku 100 za Maombi’ na marafiki zangu 90. Niliweza pia kushiriki kitabu cha ‘Pambano Kuu’ na wengi wa hao marafiki zangu. Rafiki mmoja ambaye hakuwa wa kanisa la Waadventista wa Sabato aliniomba tujifunze naye unabii wa Danieli na Ufunuo.”
  • Gloria D.: “Mungu ametubariki kuweza kuendesha program yetu ya kusambaza vyakula pamoja na kuwepo kwa ugonjwa huu wa virusi vya corona.
MAMBO YA KUOMBEA1. Ombea washiriki wote duniani ambao wanaanzisha vituo vya mvuto vya Matumaini ya Uzima.
2. Omba kwa ajili ya watu wa visiwa vya Fiji na Vanuatu ambao wameathirika hivi karibuni na kimbunga.
3. Ombea taasisi zetu za elimu kote ulimwenguni. Omba kwamba waweze kupata namna ya kutoa elimu ya Kikristo kupitia katika madarasa ya mtandao na njia zingine zozote. Omba kwamba waweze kuendelea kuwa na mvuto chanya wa kiroho kwa wanafunzi, na kuweza kubakia imara kifedha.




 

Siku ya 45 – Kitovu cha Maombi – Jumapili, 10 May 2020 
Huduma ya Yesu“Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia
wakati wa mahitaji.”
Waebrania 4:14-16


“Mwana wa Mungu… ametimiza kiapo chake, na amepita kwenda mbinguni, kupokea ufalme wa majeshi ya mbinguni. Alitimiza awamu ya kwanza ya ukuhani wake kwa kufa msalabani kwa ajili ya wanadamu walioanguka dhambini. Sasa hivi anatimiza awamu nyingine ya kuwaombea kwa Baba wale wenye dhambi waliotubu,
akiwasilisha kwa Mungu matoleo ya watu wake. Akiisha kuchukua asili ya binadamu, na hiyo asili ikashinda majaribu ya yule adui akiwa na ukamilifu wa kimbingu, yeye amepewa kuuhukumu ulimwengu. Mambo ya kila mtu yataletwa hukumuni mbele zake. Yeye atatamka hukumu, akimpatia kila mtu sawa sawa na kazi zake.” Manuscript 42, 1901

Maswali kwa Undani wa Moyo: Yesu alikuwa mwanadamu, akafa na kufufuka, na sasa hivi amesimama katika hekalu la mbinguni kama mwakilishi wa wote waliokabidhi maisha yao kwake. Unapoomba, anakusikia. Unapoomba msamaha wa dhambi, na ushindi, Anasikia na atakupatia mara moja nguvu inayohitajka ili upate kushinda. Kadiri unavyoishi katika nuru ya hukumu, je, umemfanya Yesu aliye Kuhani Mkuu mwenye huruma awe ni Wakili wako (1 Yohana 2:1)? Umetafuta mahali pa kukimbilia katika haki yake? Je, utakataa asikufunike kwa haki yake, lakini pia
asikujaze na haki yake kwa kufanya kazi alizokutayarishia (Waefeso 2:10)?


TAARIFA ZA SIFA:
  • Sheril M.: “Ninamshukuru Mungu! Hizi ‘Siku 100 za Maombi’ zimeimarisha Imani yangu wakati huu mgumu.”
  • Rose S.: “Kwa sababu ya hili gonjwa la corona, ‘Kikundi chetu cha mawasiliano ya maombi’ kimekuwa hai kadiri tunavyokuwa na muda wa kuomba pamoja kwenye mtandao mara 5 hadi 7 kila siku!”
MAMBO YA KUOMBEA1. Omba kwa ajili ya wale wasio na makazi katika majimbo yote ulimwenguni, wale ambao wanategemea wingi wa watu ili wasaidike lakini sasa wamekata tamaa kwa sababu ya kufungiwa wasitoke nyumbani.
2. Waombee wazee ambao hawawezi kujiunganisha na familia zao wakati wa zahama hii. Omba kwa ajili ya wale wanaopambana na magonjwa kama ‘dementia’ na kila aina ya kuchanganyikiwa hasa wakati huu.
3. Ombea ndoa ambazo wakati huu ziko kwenye msongo wa ziada. Omba kwamba wanandoa wanaohangaika wapate uponyaji, wapate msaada na kunyenyekea kadiri wanavyojielekeza kwa Yesu.



Siku ya 46 – Kitovu cha Maombi – Jumatatu, 11 May 2020 
Upendo wa Yesu“Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu.” Yohana 15:9

“Ikiwa nitaokolewa katika ufalme wa Mungu, nitadumu kutafakari kina kipya katika mpango wa wokovu. Watakatifu wote watakaokombolewa wataona na kukubali upendo wa Baba na wa Mwana kuliko wakati mwingine wowote, na wimbo wa sifa utalipuka kutoka katika ndimbi za wenye uhai. Alitupenda, akatoa maisha yake kwa ajli yetu. Tukiwa na miili ya utukufu, tukiwa na uwezo wenye upeo mpana, tukiwa na mioyo safi na midomo isiyo na uchafu, tutaimba utajiri wa upendo uliotukomboa.”
Letter, 27, 1890

Maswali kwa Undani wa Moyo: Mungu ni Pendo, yeye ndiye chimbuko la upendo. Haiwezekani kukawa na upendo safi kuliko upendo uliopo kwa Mungu Baba. Ikiwa Yesu alitupenda kwa upeo ambao Baba alimpenda Yeye, uwezekano ni upi wa kuvutiwa naye kuliko kuwa naye kwa upatanifu mkamlifu? Upendo wa Yesu hauna mfano! Je, sasa hivi kuna mambo katika maisha yako unayoyapenda kuliko kumpenda Yesu? Je, kuna kitu ambacho kimeteka namna moyo wako unavyovutiwa? Mwombe Yesu akuguse na upendo mkamilifu, ule anaoutumia kukupenda. Kwa nini
leo hii usichague kuukubali upendo wake moyoni mwako na kuufanya uwe ndiyo msukumo wa juu katika kutembea kwako kwa Imani?


TAARIFA ZA SIFA:
  • Baadhi ya nchi na majimbo kule Marekani yameanza kufunguka kwa ajili ya biashara (kwa kuzuiliwa).
  • Kiwango cha maambukizi na vifo kimepungua kuliko ilivyokadiriwa hapoawali.
MAMBO YA KUOMBEA1. Ombea miradi mbalimbali ya majengo kama vile makanisa na mashule kote ulimwenguni. Omba kwa ajili ya kuendelea kutoa matoleo kwa uaminifu katika zaka na sadaka.
2. Omba kwa ajili ya watu wa visiwa vya Saint Vincent na Grenadines ambao wanakabilia na ukame mbaya kuwahi kutokea unaoongezea athari ya ugonjwa huu wa virusi vya corona. Ombea mvua na mibaraka ya Mungu kwa utume wa makanisa mahalia.
 
3. Ombea washiriki ambao wamekumbwa na hali ya hofu wakati wa zahama hii.
4. Omba kwamba watu watambue tofauti kati ya kufuata kanuni za usafi zianazotangazwa na serikari na kuhimizwa kwa ibada isiyo sahihi.



Siku ya 47 – Kitovu cha Maombi – Jumanne, 12 May 2020 
Imani ya Yesu“Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.” Ufunuo 14:12

“Imani katika uwezo wa Kristo wa kutuokoa kwa upeo mkubwa na kwa ujazo na ukamilifu ndiyo Imani ya Yesu.” 3 SM 172.3


Maswali kwa Undani wa Moyo: Tunaishi katika wakati wa siku za mwisho. Huu ndio wakati kuliko wakati mwingine wowote, ambapo kutumainia uwezo wa Mungu wa kutuvusha kunahitajika. Yesu ametoa maisha yake, kifo na ufufuo na Neno lake likiwa na ahadi zake na maelekezo kwa ajli yako. Ameweka nadhiri kwa kazi ya kukuokoa, Ni jambo la ajabu au siyo?

Je, unatamani kwa dhati kuamini hivi na kukubali uhalisia huu pamoja na matokeo yake yanayobadilisha katika maisha yako? Je, ungependa Yesu achukue Imani yako iliyo ndogo na dhaifu apate kuibadilisha na kuifanya ni Imani isiyotingishika? Kwa nini usimwombe afanye kazi hii ndani yako kadiri uanvyofuata mapenzi yake siku kwa siku?


TAARIFA ZA SIFA:
  • Ni jambo la kutia moyo tunaposikia idadi ya makanisa, wachungaji, wazee wa makanisa, na washiriki wengine wanapokuwa wabunifu wakitumia fursa kufanya ibada, usharika na maombi kwa ajili ya washiriki wao kupitia kwenye mtandao bila kukoma.
MAMBO YA KUOMBEA1. Ombea miradi mbali mbali ya utume na mikutano ya uinjilisti kule Sulawezi Kaskazini katika nchi ya Indonesia.
2. Ombea wanafunzi wa Kiadventista walioko Cairo nchini Misri wanaopambana kupata chakula cha msaada kutoka kwa washiriki kwa sababu ya kuzuiliwa.
3. Ombea washiriki walio jasiri katika jimbo la Kaskazini Magharibi mwa Nigeria ambao wanashikilia ujumbe wa injili pamoja na hatari inayotokana na makundi ya magaidi, majambazi na wahalifu ambao ni wengi katika himaya hiyo.
 
4. Ombea wanafunzi waliopo Ufilipino wanaokabiliana na masuala yanayohusu masomo yao siku ya Sabato kulingana na mpango mpya uliopendekezwa wakati huu wa ugonjwa wa virusi vya corona.


Siku ya 48 – Kitovu cha Maombi – Jumatano, 13 May 2020 
Kuwepo kwa Yesu“Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.” Yohana 16:7 “…na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” Mathayo 28:20

“Kuanzia hapo, Yesu alidumu katika mioyo ya watoto wake kupitia kwa Roho. Huu muunganiko pamoja naye ulikuwa wa karibu kuliko wakati akiwepo kimwili pamoja nao. Nuru, upendo na nguvu ya kuwepo kwa Kristo viliangaza kupitia kwao, ili watu walipoona, ‘… na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.’” Matendo 4:13
..Steps to Christ, uk. 74.1

Maswali kwa Undani wa Moyo: Je, umewahi kutamani kama ungekuwa hai wakati Yesu alipokuwa hapa duniani? Kutembea na kuongea naye? Lengo la injili lenye nguvu ni kukupatia kitu fulani kilicho bora zaidi! Yesu anapenda aishi ndani yako, akikufanya ufanane naye kupitia katika huduma ya Roho Mtakatifu ibadilishayo. Je, umewahi kumwomba Yesu akubatize kwa Roho Mtakatifu ili upate kuhisi na kuona kuwepo kwake ndani yako? Yesu alituambia kuwa tuombe kipawa cha Roho Mtakatifu kila siku (Luka 11:13). Kwa nini usimkaribishe Kristo sasa hivi, afanye makao ndani yako kupitia kwa Roho Mtakatifu?

TAARIFA ZA SIFA:
  • Watu wengi sana wanaotuzunguka ni wepesi kupokea ushuhuda wetu na uelewa wa Maandiko kwa sababu ya zahama hii. Tumsifu Mungu kwa kuwa anaokoa wengi kwa umilele pamoja naye wakati huu wa ugonjwa wa virusi vya corona unaoangamiza wengi.
MAMBO YA KUOMBEA1. Ombea wale watu wanaoshughulika na ukandamizaji wa mapepo na kupagawa.
Omba kwamba wafunguliwe kutoka katika nguvu za Shetani. Ombea familia zao,
hasa watoto wenye wazazi walioathirika. 

 2. Omba kwa ajili ya maelfu ya vikundi na makanisa yaliyoanzishwa ulimwenguni kote ili yaendelee kuwa imara na hai pamoja na uwepo wa adha hii ya ugonjwa wa virusi vya corona.
3. Ombea wachungaji na viongozi wa makanisa katika nchi ambazo zina huduma mbaya ya afya.
4. Omba kwa ajili ya vituo vya radio za Kiadventista vinavyowafikia wale wasiofikiwa ulimwenguni kote.


Siku ya 49 – Kitovu cha Maombi – Alhamisi, 14 May 2020 
Huruma ya Yesu“Bwana ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema.” Zaburi 116:5
 

“Roho zilizokuja kwa Yesu zilihisi uwepo wake hata wakaweza kuepuka shimo la dhambi. Mafarisayo waliwakataa na kuwadharau, lakini Kristo aliwasalimu kama watoto wa Mungu waliotenganishwa kutoka katika nyumba ya Baba, lakini ambao hawakusahauliwa na moyo wa Baba. Na huzuni zao, na dhambi zao ziliwafanya wawe walengwa wa huruma zake. Kadiri walivyotanga mbali kutoka kwake, ndivyo walivyozidi kutamani, lakini pia ndivyo kafara ya wokovu wao ilivyozidi kuwa kubwa.” Christ’s Object Lessons, uk. 186.2

Maswali kwa Undani wa Moyo: Neema ya Mungu kwetu ni matokeo ya huruma yake kuu kwa wote wanaoteseka chini ya dhambi, na mambo yanayoambatana na dhambi. Ukitambua huruma yake kwako, kwa namna inavyooneshwa katika Yesu, ni nini kinachokuzuia kuja kwake jinsi ulivyo, na kukabidhi kwake leo hii pembe zote zenye giza katika maisha yako? Yesu anaelewa fika mizigo uliyo nayo, jinsi unavyopambana na majaribu. Yuko tayari kabisa kukusaidia, kukuponya, kukusamehe, kukuinua, na kukutegemeza. Je, hauwezi kuruhusu leo hii upendo wake, neema yake, na huruma zake
ziyeyushe namna yoyote unayohisi ya kumkataa au kutokumjali?


TAARIFA ZA SIFA:Waadventista wengi pamoja na Wakristo wengine wanatambua kwamba tumebweteka mno na kuendesha makanisa yetu kwa namna ya kibinadamu. Tunahitaji wito wa kutuamsha na kutusaidia kuishi maisha ya Imani, maombi, na miujiza kama kanisa la awali walivyofanya katika kitabu cha Matendo ya Mitume. Wakati ule waumini hawakuwa na fedha, hawakuwa na digrii, nyumba wala taasisi, lakini kwa sababu ya majaribu na hata mateso, kwa uwepo wa nguvu za Roho Mtakatifu walipindua dunia na kupeleka injili ulimwenguni kote kwa kipindi cha miaka michache tu.

MAMBO YA KUOMBEA1. Ombea makanisa kule Jamaica. Omba kwa ajili ya washiriki ambao wanakabiliana na ugumu wa hali ya kifedha, pamoja na watendakazi wa Andrews Memorial Hospital, na waginjwa hasa wakati huu wa ugonjwa mbaya wa corona.
2. Ombea washiriki wa kanisa na wana familia wanaohangaika na uraibu wa picha za ngono, pombe, sukari, filamu mbaya, miziki, na vilevi vingine pamoja na mienendo potovu. Omba kwamba wapate ushindi katika Kristo.
3. Omba kwa ajli ya kanisa la kusini mwa Windhoek kule Namibia ambao wamekuwa wakijaribu kupata kibali cha kununua ardhi ili wajenge kanisa bila mafaniko kwa kipindi cha miaka kumi, Mungu afungue njia.
4. Omba kwa ajili ya kiwanda cha kuoka mikate kule Granna nchini Sweden waweze kuwafikia wengi katika mji wao kwa ujumbe wa injili.
Share:

No comments:

Post a Comment

Translate

Categories

USOMAJI WA BIBLIA KWA MPANGO

...

BUSEGWE GIRLS HIGH SCHOOL

Tunapokea wanafunzi Kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 2021 kuanzia tarehe 7 Januari.
Pia nafasi za wahamiaji kidato cha tano zipo!
NYOTE MNAKARIBISHWA
Mawasiliano: +255759346439 (Mkuu wa Shule)
+255745114360 (Mhazini)

Support

Kanisa letu ni kanisa la shule ya sekondari ya wasichana Busegwe, katika jimbo la Mara. Shule hii ina uhitaji mkubwa wa kifedha kwa ajili ya maendeleo. Hivyo, kwa unyenyekevu, tunasihi sapoti yako ilikuweza kuiendeleza na kufanikisha programu mbalimbali ikiwemo uinjilisti.

Wasiliana nasi kwa mawasiliano yaliyo tolewa hapo chini au bofya HAPA