UNIONI YA KASKAZINI MWA TANZANIA
CHAMA CHA WACHUNGAJI/HUDUMA ZA MAOMBI
SIKU 100 ZA MAOMBI:
MACHI 27 – JULAI 2, 2020
“Kumlilia Yesu wakati wa Uhitaji wetu mkuu!”
Masomo haya yameandaliwa na Mark Finley ambaye ni Msaidizi wa Halmashauri Kuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato
Yametafsiriwa na Moseti Chacha na kuratibiwa na Huduma za Maombi NTUC.
Wakati wa Kujichunguza MoyoNa Mark Finley“Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu; Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele..” – Zaburi 1 39:23:24
Miaka kadhaa iliyopita, mapema kabisa katika huduma yangu, niliitwa kuendesha juma la msisitizo wa kiroho kama Mkristo katika shule ya awali. Kadiri juma lilivyoendelea ilionekana wazi kwangu kuwa, walimu wawili walikuwa na mtafaruku mkubwa kati ya walimu wote waliokuwa pale. Mara nyingi tofauti zao zilifukuta hata kujitokeza katika mikutano ya walimu. Mmoja alipopendekeza wazo fulani, mwingine alilipinga. Nyakati ambazo wote walihudhuria kwenye mkutano wa waalimu, kulijitokeza mivutano isiyokuwa na maana. Ni dhahiri kwamba hakuna aliyekuwa akimpenda mwenzake kabisa.
Karibu na mwisho wa juma, nilihubiri kuhusu ombi kuu la upatanisho la Yesu katika sura ya 17 ya kitabu cha Yohana. Yesu alipokaribia kuachana na wanafunzi wake. Muda mfupi ujao angesalitiwa na kusulubiwa. Angefufuka kutoka kaburini na kupaa kwa Baba yake. Ombi lake la dhati liliakisi kile kilichokuwa ndani ya moyo wake. Ombi hilo lilidhihirisha kile kilichokuwa katika fikra zake kabla tu ya kifo chake pale msalabani. Mwokozi alikuwa akisumbuka kuhusu umoja wa kanisa. Aliomba kuwa, “Wote wawe na umoja; kama wewe Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.” (Yohana 1 7:21 ). Kristo alitamani kuwa mafarakano, wivu, kuhangaikia ukubwa, na migogoro kati ya
wanafunzi wake vyote vikome. Aliomba kwamba pamoja na tofauti zote hizo, umoja wao uoneshe uwezo wa upendo wake ulimwenguni.
Nilipokuwa nikiwashirikisha wanafunzi na waalimu jinsi moyo wa Kristo unavyotamani, jambo lisilo la kawaida lilitokea. Usiku wa mwisho wa juma hilo la msisitizo wa kiroho, tulipanga kuwa na huduma ya kuoshana miguu kisha meza ya Bwana. Roho Mtakatifu akaingilia kati. Mungu akawagusa kwa namna kuu. Wale waalimu wawili waliokuwa na mtafaruku walioshana miguu. Roho wa Mungu akavunja kuta za utengano. Wakakumbatiana, wakaungamiana mwenendo wao wa mtazamo hasi na hatimaye wakaomba pamoja.
Wanafunzi wa Yesu walipitia uzoefu kama huo, uliohusu toba na unyenyekevu katika zile siku 1 0 walipokuwa chumba cha juu ghorofani wakisubiri Pentekosti. Katika kipindi kile cha siku kumi, wanafunzi waliungamiana tofauti zao ndogo ndogo wao kwa wao. Walitubu wivu wao na kiburi chao. Mioyo yao ilijawa na upendo kwa Kristo ambaye alikuwa ametoa yote kwa ajili yao. Ni kwa namna gani walikuwa wakitamani kuwa wangeishi tena maisha kama haya miaka mitatu na nusu illiyopita.
saa ya maisha nyuma, ukarudi kutengeneza makosa ya zamani?
Tunapoona wema wa Mungu wenye upendo, na kutambua haki ya tabia yake, tunagundua udhaifu wetu, mapungufu, na dhambi zetu. Katika mng’ao wa nuru ya upendo wake usiokuwa na masharti pamoja na ukamilifu wake, mioyo yetu inanyenyekezwa. Tunaongozwa katika toba ya kina na maungamo. Tunamlilia apate kutuokoa na kutuhesabia haki ambayo ni yeye pekee anayeweza kutoa. Tunapozidiwa na ule utakatifu wake, tunaungana na nabii Isaya tukilia kwamba, “Ole wangu! Kwa
maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu…” (Isaya 6:5) Katika kujichunguza wenyewe tunamuuliza Mungu kuwa, “Je, kuna jambo lolote katika maisha yangu ambalo haliko sawa sawa na mapenzi yako?” Ndipo tunaomba kwa maneno haya: “Bwana nakuomba udhihirishe mwenendo ndani ya nafsi yangu ambao haufanani na Yesu.”
Lengo la Mungu katika mchakato wote huu ni kutuongoza karibu naye. Hahitaji watu kugaagaa katika hatia au kujazwa na majuto kwa maisha yetu yaliyopita. Lengo lake ni kutuongoza “katika njia ya milele.” Ingawaje ni jambo lenye ustawi kurudi na kutazama upya maisha yetu ya kiroho, hata hivyo siyo jambo lenye ustawi kudumu katika makosa ya maisha yetu yaliyopita. Kudumu katika makosa yetu yaliyopita na kujielekeza katika makosa hayo kwa kipindi kirefu kutaendelea kutukatisha tamaa tu.
Kumbuka kwamba siku zote Bwana wetu ni mkuu kuliko makosa yetu, na ni mkuu kuliko kushindwa kwetu. Ni dhahiri kwamba tunahitaji kufahamu hali yetu wazi wazi – lakini ni muhimu zaidi kufahamu neema Yake. Kuelewa udhaifu wetu kunatutayarisha kupokea nguvu zake. Kufahamu vyema hali yetu ya dhambi kunatutayarisha kupokea haki yake. Kuelewa vyema ujinga wetu kunatutayarisha kupokea hekima yake. Kusudi kubwa la ushawishi wa Roho ni kutuongoza kwa Yesu. Kadiri tunavyotambua dhambi zetu na makosa yetu kupitia katika mchakato wa kujichunguza au kujitathmini, tunaweza kumshukuru Mungu kwamba Roho wake Mtakatifu anatuongoza karibu ya Yesu, na kwa namna hiyo kutuvuta karibu sisi wenyewe kila mmoja kwa mwenzake. Ile nguvu ya Roho Mtakatifu inayoshawishi, inatutayarisha kupokea kwa ukamilifu Roho katika nguvu ya mvua ya masika. Lakini kabla Mungu hajatutengeneza, ni lazima atuvunje vunje. Kabla hajatujaza, ni lazima kwanza atufanye watupu. Kabla hajatuinua katika kiti cha enzi mioyoni mwetu, ni lazima aondoe kiburi kutoka katika mioyo yetu.
Mark Finley ni Msaidizi wa Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya kanisa la Waadventista
wa Sabato.
Maswali kwa Undani wa Moyo: Moyo wako leo uko wapi? Je, umewahi kupitia uzoefu wa zawadi tamu ya toba? Ikiwa ni hivyo je, unaona kama maisha yako yamebadilika kutoka katika hali uliyokuwa nayo hapo awali? Umepata uzoefu wa neema ya Mungu kwa namna iliyo mpya? Je, umejifunza kuendeleza neema hiyo kwa wengine?
Changamoto ya Moyo iliyo hai: Mwombe Mungu adhihirishie yale mambo yanayochukua muda wako katika maisha yako, mambo yanayoteka shauku yako, na yale yote yanayoondoa mivuto yako kutoka kwa Yesu. Kadiri unavyofikiria aya za Isaya 59:12 na 1 Yohana 1:9, omba na kumwambia Mungu adhihirishe nyufa zozote za kiroho ambazo zinaweza kuwa katika maisha yako. Omba kwamba aziondoe, na kukupatia hisia za kina za kujazwa na Roho Mtakatifu.
ya nje, kwa sababu wanaogopa kwamba matendo yao mabaya waliyotenda yataleta
mateso juu yao wenyewe. Lakini huku si kutubu kwa maana ile ya Biblia. Wao huomboleza kwa ajili ya mateso wanayopata kuliko kwa ajili ya ile dhambi waliyotenda. [Hayo yalikuwa ndiyo majuto ya Esau alipoona ya kwamba alikuwa ameupoteza urithi wake milele. Balaamu, alipotiwa hofu nyingi sana kwa ajili ya kumwona malaika aliyesimama mbele yake na upanga mkononi mwake, alikiri kosa lake asije akapoteza maisha yake; lakini hakutubu kwa kweli, nia yake haikugeuka, yaani, hakuchukizwa na yale maovu. Yuda Iskariote, baada ya kumsaliti Bwana wake, alisema, “Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia]…
Daudi aliuona ukubwa upitao kiasi wa kosa lake; aliona unajisi wa moyo wake; aliichukia
sana dhambi yake. Hakuomba ili apate msamaha tu, aliomba pia ili awe na moyo safi.
Alitamani sana kuwa na furaha iletwayo na utakatifu - yaani, kurejeshwa katika hali ya amani na ushirika na Mungu.” Steps to Christ, uk. 23-25
Kuingia kwa undani – Mapendekezo ya Masomo ya ziada kwa Juma hili.
Ellen G. White, Steps to Christ, sura ya 3, “Kutubu.”
Mark Finley, 10 Days in the Upper Room.Siku ya 57 – Kitovu cha Maombi – Ijumaa, 22 May 2020Taarifa za Sifa!
• Jinia Y.: “Ninamsifu Mungu kwa ajili ya Huduma ya vyombo vya Habari. Mahubiri pamoja na shuhuda ambazo tunasikiliza na kutazama kwenye mitandao zimenisaidia kukabiliana na maumivu niliyokuwa nayo wakati huu wa kutengwa.”
ya kuitikia.”
MAMBO YA KUOMBEA
1. Ombea maeneo ambapo ugonjwa huu wa virusi vya corona unaonekana kuanza tena, kama vile Wuhan kule China na maeneo mengine ya miji na majimbo ya China.
2. Ombea waalimu wa Kiadventista katika shule zinazoendeshwa na serikali kule Thailand. Kuna uwezekano kwamba shule zitakapofunguliwa, serikali italazimisha masomo siku ya Jumamosi ili kufidia muda uliopotea. Omba kwa ajili ya kuimarika kwa Imani ya waalimu na kwamba wasimame imara kwa jinsi wale rafiki zake Danieli walivyosimama.
3. Ombea vikundi vidogo vidogo, makanisa ya nje, na mikutano ya kiinjilisti ambayo imeanzishwa kote katika Papua New Guinea kwa sababu ya kufungwa kwa makanisa.
4. Ombea huduma ya kanisa la Waadventista wa Sabato ya kituo cha Omega katika sehemu ya New Heaven, Connecticut kule Marekani, kinachohudumia watu wasiokuwa na makazi waweze kudumisha nafasi kwa kila mmoja ili kuepuka ugonjwa huu wa virusi vya corona.
Siku ya 58 – Kitovu cha Maombi – Jumamosi, 23 May 2020
Umaskini Wenye Mibaraka
“Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.” – Mathayo 5:3
“Wale wanaofahamu kwamba hawawezi kujiokoa wenyewe, au kutenda tendo lolote la haki, hao ndio wanaofurahia msaada ambao Kristo anawapatia. Hao ndio maskini wa roho, ambao anawataja kuwa wenye heri. Hao ndio ambao Kristo amewasamehe, kwanza anawafanya watubu, na kazi hiyo ya kuwafanya hivyo ni kazi ya ofisi ya Roho Mtakatifu ambaye anawashawishi waone kwamba hakuna jambo jema ndani yao wenyewe. Wanaona kwamba kila jambo walilofanya limechanganyika na ubinafsi pamoja na dhambi. Kama yule mtoza ushuru aliyesimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, wanasimama mbali na kuijipiga-piga kifua wakisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi’ …Wale wote wenye hisia kwa kina za upungufu wao, wale wanaojisikia kwamba hawana kitu chema ndani yao, watapata haki na nguvu kwa kumtazama Yesu.” Thoughts from the Mount of Blessing, uk. 7-8
Kwa nini leo usije kwa Yesu jinsi ulivyo, pamoja na kiasi chochote ulichovunjika, hata na ubinafsi wenye dhambi? Kwa nini usidai tu damu yake, uhai wake, na kifo chake kama njia ya wokovu? Kwa nini usimuulize Yesu ang’oe ile hali ya kujiamini na kujitegemea ambayo bado imo ndani ya moyo wako, badala yake aweke Imani katika uwezo wake wa kukuokoa, na kukuwezesha kutenda kazi njema zinazohamasishwa na upendo usiokuwa na ubinafsi?
TAARIFA ZA SIFA:
• Nolubabalo D.: “Ahsante sana Bwana kwa mkono wako unaoonekana Afrika.
Ahsante sana kwa ulinzi wako. Ahsante sana kwa kuwalinda watoto wangu wakati nilipokuwa sipo. Unastahili kusifiwa.”
• Philippe M.: “Katika mji wetu wa Kananga hatukuwa na matangazo ya radio kabla ya kutangazwa kwa amri ya kubakia majumbani, lakini wakati huu wa janga hili tunavyo vituo vinne vinavyorusha matangazo kila juma kupitia katika radio nne mahalia. Tunamsifu Mungu kwa yote hayo!”
MAMBO YA KUOMBEA
1. Mwombe Yesu akusafishe kutokana na hali ya kujihesabi haki na akupatie kutambua kuwa kila siku na maisha yako yote unamhitaji Yeye sana.
2. Waombee wainjilisti kule Afrika Kusini ambao wanapambana na masuala mbalimbali ya kiafya na misongo. Omba kwamba waponywe na kuwezeshwa kupata namna ya kuhubiri injili pamoja na hali ilivyo.
3. Mwombee ndugu Samuel S. anayeumwa ugonjwa unaompa maumivu makali katika sehemu chini ya mwili wake na madaktari hawajagundua tatizo linalomsibu. Mwombee pia dada Tabitha N. ambaye ameonekana kuwa na tundu kwenye moyo wake na anapitia kipindi cha maumivu makubwa. Ombea uponyaji wao na wengine wengi ambao wanaugua magonjwa mbalimbali wakati huu.
mafundisho ya Biblia
Siku ya 59 – Kitovu cha Maombi – Jumapili, 24 May 2020
Huzuni Zimevunjwa“Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika.” Mathayo 5:4
“Huzuni inayotajwa hapa ni huzuni ya moyo kwa ajili ya dhambi… Na kwa jinsi mtu anavyovutwa kumwangalia Yesu akiinuliwa msalabani, anatambua hali ya binadamu ya dhambi. Anaona kwamba ni dhambi ndizo zilimfanya Bwana wa utukufu akapigwa mijeledi na kusulubiwa. Anaona kwamba pamoja na kupendwa kwa upendo usiopimika, maisha yake yamekuwa ni mwendelezo wa uasi na ukosefu wa shukurani. Amemkataa yule aliyekuwa rafiki wake wa karibu na kuitukana zawadi ya thamani kutoka mbinguni. Amemsulubisha mwana wake wa pekee yeye mwenyewe na kuuchoma upya ule moyo uliokuwa ukivuja kwa mapigo. Ametengwa na Mungu kwa ufa mkubwa wa dhambi ambao ni mpana na mweusi na wenye kina kirefu, na ana huzuni ya kuvunjika moyo. Huzuni ya jinsi hii itapata kufarijiwa. Mungu anadhihirisha hatia yetu ili tumkimbilie Kristo, na kupitia kwake tuwekwe huru kutoka katika kongwa la dhambi, na kufurahia katika uhuru wa mwana wa Mungu. Kwa majuto ya dhati tunaweza kuja chini ya msalaba, na hapo tukatua mizigo yetu.” Thoughts from theMount of Blessing, uk. 9-10,
TAARIFA ZA SIFA:
• Diane T.: “Kumsifu Mungu kwa fursa ya kuhudhuria Kambi la Biblia kwa mtandao. Kumekuwa na mibaraka mingi wakati huu.”
• Iris R.: “Nilikuwa mraibu wa kuangalia Binge Netflix. Nilikuwa najaribu kusoma mistari kadhaa katika Biblia ili kujihalalisha, na kisha kuendelea kuangalia. Baada ya maombi ya juma moja shuleni kwetu Mungu alinionesha kwamba nahitaji kufuta program tumishi zinazohusiana na Binge Netflix. Baada ya muda nilirudi kuangalia filamu za Biblia, lakini sikuweza kujitawala, nilirudi tena katika utawala wa Shetani. Nilimlilia Mungu. Siku iliyofuata mchungaji alinipatia Biblia aina ya ‘Andrews Study Bible’ kama zawadi. Nilifurahi sana hadi machozi yalitiririka nikimshukuru Mungu kwa kuingilia kati.
Alinikumbusha aya ya Wafilipi 2:13 inayosema kuwa, “Kwa maana ndiye Mungu
atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi
lake jema.” Ninamsifu Mungu kwa kunibadilisha na kunijaza ahadi zake.
MAMBO YA KUOMBEA
1. Omba kwa ajili ya uelewa dhahiri wa kile kilichotokea pale msalababi. Omba kwamba Mungu akusaidie kuchukia dhambi na kupenda haki.
2. Ombea kazi ya uuzaji wa vitabu kule Malawi pamoja na namna ya kuwategemeza kifedha ili waanzishe kituo cha uponyaji (sanitarium) na kazi za umisionari wa matibabu katika jimbo hilo.
4. Ombea washiriki wa kanisa la Waadventista wa Sabato wa Peter’s Rest katika visiwa vya Croix na Virgin. Jengo lao la kanisa liliungua na kuteketea kabisa. Omba kwamba wapate hekima ya namna ya kuanza upya na kuendelea ili hasara hii ibadilishwe na kuwa ushindi kwa Yesu.
Siku ya 60 – Kitovu cha Maombi – Jumatatu, 25 May 2020
Kuzawadia Unyenyekevu“Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.” Mathayo 5:5
“Asili ya binadamu siku zote inapambana kujitokeza, tayari kwa mahojiano, lakini yeye ajifunzaye kwa Kristo anaondolewa ubinafsi, kiburi, kupenda ubwana, na anakuwa na utulivu nafsini mwake. Ubinafsi unajiachia kwenye uwepo wa Roho Mtakatifu. Ndipo tunapopoteza shauku ya kutaka ukubwa. Tunakosa tamaa ya makuu ili kujitokeza tuonekane; lakini tunaona kuwa mahali petu pa juu sana ni miguuni pa Mwokozi. Tunamwangalia Yesu, tukisubiri mkono wake utuongoze, tukisikiliza sauti yake ituongoze.” Thoughts from the Mount of Blessing, uk. 15
Maswali kwa Undani wa Moyo: Hakuna mahali penye furaha maishani kuliko kufahamu
kwamba unao upatanifu mkamilifu na Mungu katika mambo yote yale utendayo. Huu
upatanifu unakuwepo pale Yesu anapotafutwa, na ile hali ya kujikweza ikatupiliwa mbali, ukitambua kwamba “Moyo (wenye dhambi) huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una
ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua”
Je, utamuomba Yesu akuondolee tamaa ya kiburi na majivuno, tamaa ya kujiangalia kwa ubinafsi, na upendo wako wa ukuu? Utamwomba akuwezeshe kubadilisha hayo mambo kwa kukuwezesha kufanyia kai upole, unyenyekevu, na wema kuanzia leo?
TAARIFA ZA SIFA:
• Claudia P.: “Ninamsifu Mungu kwa rehema zake ambazo ni mpya siyo kila asubuhi tu bali wakati wote! Amekuwa mwema kwa familia yangu na mimi mwenyewe zaidi ya namna ambavyo maneno yanaweza kuelezea. Ninamsifu Bwana!”
• Rose K.: “Msifu Mungu kwa haya maombi ya siku 100! Kila siku ninasukumwa kufanya kitu kipya au kuona mabadiliko mapya kwa waumini wengine. Baadaye ninatambua kwamba kile nilichoona kwa kweli kilikuwa ni jibu kwa ombi fulani katika maombi haya ya siku 100. Ni jambo la kushangaza kuona jinsi Roho Mtakatifu anavyofanya kazi.”
MAMBO YA KUOMBEA
1. Omba kwamba Yesu akufanye mpole na mnyenyekevu
2. Ombea washiriki kule Uganda ambao wameathiriwa na mafuriko. Mafuriko yamesababisha nyumba nyingi kuanguka na kuharibika. Wengi hawana makazi na hasa kati ya hili janga ambalo katika nchi hiyo limesababisha kutokuruhusiwa kutoka majumbani mwao.
3. Omba kwa ajili ya waalimu Waadventista kote ulimwenguni wanapopitia katika ugumu wa kifedha kwa sababu ya kutokuweza kufanya kazi.
4. Omba kwa ajili ya vijana ili watambue umuhimu wa kumtumikia Mungu na siyo kuutumikia ulimwengu.
Siku ya 61 – Kitovu cha Maombi – Jumanne, 26 May 2020
Lishe ya Mwenye Haki“Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.” Mathayo 5:6
“Haki ni utakatifu, inafananishwa na Mungu, na ‘Mungu ni upendo’ 1 Yohana 4:16. Ni hali inayokubaliana na sheria ya Mungu, ‘… Maana maagizo yako yote ni ya haki’ (Zaburi 119:172) na ‘…pendo ndilo utimilifu wa sheria’ (Warumi 13:10). Haki ni Upendo, na upendo ni nuru na uzima wa Mungu. Haki ya Mungu imeunganishwa katika Kristo. Tunapokea haki kwa kumpokea Yeye.” Thoughts from the Mount of Blessing, uk.18
kupata zawadi mbili za neema iletayo haki:
1 . Kuhesabiwa haki, ambayo ni ahadi kwamba unafunikwa na maisha yake makamilifu kupitia katika Imani kwenye hiyo ahadi.
2. Kupewa haki, ambayo ni ahadi kwamba atakubadilisha kutoka katika kuwa mwenye ubinafsi hadi kuwa kiumbe unayeakisi upendo wa Yesu usiokuwa na ubinafsi, kupitia katika Imani hai kwenye hiyo ahadi
Zawadi mbili hizi zitakukamilisha, zitakushibisha kwa hakika, zitakuokoa! Kwa nini
usizikubali leo hii na kuanza kuishi maisha mapya ya furaha yaliyojawa na Yesu katika
kutambua uhalisia wake unaoshangaza wa upendo wa Mungu ukomboao?
TAARIFA ZA SIFA:
• Jane D.: “Mungu amemponya mgonjwa niliyekuwa nikimwombea. Na kwa namna ya ajabu amegusa mioyo ya familia yangu.”
• Marcia N.: “Binti yangu amekuwa mraibu wa madawa ya kulevya kwa miaka mingi, ameishi bila makao, na hata akapelekwa gerezani. Vikundi vyetu vya maombi vilianza kumwombea na matokeo yake amefanikiwa kujiunga na kitengo kinachosaidia waathirika wa jinsi hii akipata msaada, na afya yake inaendelea vizuri, ameanza kuwa na shauku kwa mambo ya Mungu na anasoma vitabu vya
Roho ya Unabii. Anasema kuwa ni Mungu aliyemsaidia. Ninamsifu Mungu kwa upendo wake kwetu na jinsi alivyotusaidia katika kipindi chote cha hii miaka ya kuvunjika moyo” Vilio vinaendelea usiku, lakini furaha huja asubuhi.
MAMBO YA KUOMBEA
1 . Omba kwamba haki ya Kristo ikufunike na kukujaza.
2. Omba kwamba Mungu aingilie kati katika mlipuko wa ugonjwa wa uti wa mgongo katika jimbo mojawapo huko Ghana. Mlipuko huu tayari umeshaua watu wengi katika jimbo hilo.
3. Ombea makanisa ambayo hayajishughulishi tangu ugonjwa huu wa virusi vya corona ulipolipuka. Ombea wachungaji, viongozi wa kanisa, na washiriki wapate kufahamu namna bora ya kujiunganisha wakati huu. Omba kwa ajili ya mtazamo mpya kuhusu umuhimu wa maombi.
4. Ombea washiriki wa Myanmar kadiri wanavyojaribu kutumia mitandao kueneza injili wakati huu wa zahama
Siku ya 62 – Kitovu cha Maombi – Jumatano, 27 May 2020
Uwe na Rehema!“Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.” Mathayo 5:7
“Mungu mwenyewe ni chanzo cha rehema yote. Jina lake ni ‘…mwingi wa huruma,mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli’ Kutoka 34:6. Hashughuliki na sisi kwa namna tunayostahili. Wala haulizi kama tnastahili upendo wake, bali anamimina juu yetu utajiri wa upendo wake, ili kutufanya tustahili. Siye mwenye kulipiza kisasi. Hatafuti kuadhibu bali kukomboa… Anatamani sana kuwaondolea wanadamu adha na masumbufu yote, kuweka dawa kwenye vidonda vyake… Wenye rehema ni warithi wa asili ya kimbingu, na ndani yao ule upendo wa Mungu ulio na huruma unajidhihirisha. Wale wote wenye mioyo yenye huruma na upendo wa milele, watatafuta kuokoa wala siyo kushutumu. Uwepo wa Kristo katika nafsi zao ni chemchemi isiyokauka. Pale alipo, kutakuwa na bubujiko la wema.” Thoughts from the Mount of Blessing, uk. 22
Maswali kwa Undani wa Moyo: Chukua muda kutafakari kuhusu rehema za Mungu katika maisha yako. Anakutakika mema, bila kujali ukosefu wa uaminifu wako. Hahitaji uhakikishe kwamba unastahili ili kupokea zawadi yake ya wokovu. Anakuchukulia kwa upendo. Unapopitia katika uzoefu wa ndani wa rehema za Mungu, Roho Mtakatifu atakuwezesha kuwa wakala wa rehema; ukishughulika na wale wanaokuzunguka kwa upendo huo huo na rehema. Hasa wale ambao wamekukosea. Je, leo hii utachagua kwa msaada ya Yesu kuendeleza rehema za Mungu kwa watu
walio katika maisha yako? Kuwasamehe kabla hawajaomba msamaha, kuwapenda kabla haujapewa sababu ya kufanya hivyo? Kuwatakia mema bila kujali kama wanastahili au la?
• Elham L.: “Nimekuwa nikiomba niwe na uhusiano wa kina na Mungu. Tangu nilipojiunga na mpango wa maombi ya siku 1 00 kila siku katika ibada zangu za asubuhi nikitumia mtiririko wa jinsi ya kuomba, maisha yangu yamehuishwa. Umekuwa ni mlipuko ambao sikutazamia.
• Sherma J.: “Mungu amejibu maombi kwa mshiriki aliyepotea. Alipuuza jitihada zangu za kumwita. Nilipomtembelea, aliongelea tu kuhusu matatizo yake bila kunipa nafasi ya kuzungumza. Nilimwomba Mungu afanye kazi ndani ya moyo wake kwamba, badala ya mimi kumwita, yeye ndiye aniite. Majuma mawili baadaye aliniita na kusema kwamba matatizo yake yameisha na kwamba alitaka kurudi kanisani na kutoa maisha yake upya kwa Mungu!”
MAMBO YA KUOMBEA
1 . Mwombe Mungu akufanye kuwa wakala wa rehema zake kwa watu walioko katika maisha yako.
2. Ombea wanafunzi ambao wanahangaika kupata karo za shule ili waendelee na elimu. Omba kwamba wawezeshwe kupitia uzoefu wa uongozi wa Mungu katika elimu yao.
3. Omba kwa ajli ya watu na washiriki wa Zimbabwe. Wengi wao hawawezi kumudu kubaki majumbani mwao kulingana na amri ya kutokutoka nyumbani. Mfumo wa huduma za afya hauwezi kushughulika na janga hili la maambukizi ya virusi vya corona.
4. Ombea wachungaji kadhaa kule Indonesia walioambukizwa na ugonjwa wa corona.
5. Omba kwamba Mungu abariki mpango wa wanafunzi wa kutoka na kuwafikia watu kule Brazil unaofanyika kwa kujitolea kuzalisha vitakasa mikono kwa ajli ya wazee.
Siku ya 63 – Kitovu cha Maombi – Alhamisi, 28 May 2020
Maono Safi“Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.” Mathayo 5:8
“Roho Mtakatifu anachukua ukweli kumhusu Mungu pamoja na mwengine yeyote yule aliyemtuma, na kuuleta katika uelewa wa ndani ya moyo. Wenye moyo safi wanamwona Mungu katika uhusiano mpya ulio mzuri, kama Mkombozi wao, na wakati wakitafakari tabia yake iliyo safi na yenye upendo, wanatamani kuakisi sura yake. Wanamwona kama Baba mwenye shauku ya kumkumbatia mwana aliyetubu, na mioyo yao inajazwa na furaha isiyoelezeka yenye utukufu mkamilifu.” Thoughts from the Mount of Blessing, uk. 26
Maswali kwa Undani wa Moyo: Tunapotembea na Mungu kwa uaminifu, anaendelea kufungua macho yetu kwa uelewa zaidi na zaidi wa tabia yake ya upendo, nia yake, na uzuri wake. Katika kutambua utakatifu wake ulio mkamilifu, na usafi wake, uchafu wetu unadhihirika na tunakaribishwa kupokea utakaso ambao ni yeye pekee awezaye kuutoa. Upande huu wa mbingu tunaona kwa macho ya Imani, lakini siku moja hivi karibuni, tutamwona uso kwa uso! Hiyo itakuwa ni siku ya utukufu. Hadi hapo, kwa nini usimwombe ausafishe moyo wako kutoka katika uchafu na uovu? Kwa nini usitafute kwa dhati maono dhahiri na uelewa kutoka kwa Mungu na nia yake?
TAARIFA ZA SIFA:
• Shana S.: “Katika kipindi hiki cha Maombi ya siku 1 00 nilianza kumwombea rafiki yangu wa miaka 20 ambaye bila sababu yoyote alianza kunipuuza kuanzia mwaka 201 7. Akanifungia kwenye simu yake na mengine mengi. Nilijaribu mara kadhaa kumfikia lakini hakuitika. Kiongozi wetu wa maombi alituhimiza kumlilia Mungu. Mimi nilifanya hivyo, nikaita tena lakini hapakuwa na jibu lolote. Siku iliyofuata aliniita! Alifungua simu yake kwamba sasa naweza kumpigia na akaniambia kwamba sikuwa nimetenda jambo lolote baya. Tukarudi kuunganika tena na kupatana. Mungu alijibu maombi yetu.”
MAMBO YA KUOMBEA
1 . Omba kwa ajili ya moyo safi, uhuru kutoka katika dhambi, kusafishwa kutoka katika kila aina ya uchafu.
2. Ombea wakurugenzi wanaohusika na mazishi, wahudumu wa vyumba vya maiti, na wafanyakazi wote wanaohusika na huduma za mazishi kadiri wanavyohusika moja kwa moja wakigusana na wengi waliokufa kwa ugonjwa huu unaoambukizwa na virusi vya corona.
3. Ombea kanisa kule Fiji, kadiri wanavyofikiria kubadilisha muundo, kwa kuimarisha na kuwezesha walei kumiliki majukumu mbalimbali.
4. Omba kwa ajili ya huduma ya kanisa la Waadventista wa Sabato la ‘Harvest’ kule Alabama, Marekani. Hawa wako katika maeneo ya kipato cha chini, maeneo yenye vitendo vingi vya jinai, na watu wachache wanoongoka kwa jitihada za kuongoa roho. Waombee kwamba Mungu alete namna ya kujikwamua.
No comments:
Post a Comment