BUSEGWE GIRLS' HIGH SCHOOL

Tunapokea wanafunzi Kidato cha kwanza hadi cha nne kuanzia tarehe 7/1/2021 Pia nafasi za wahamiaji kidato cha tano zipo!
Mawasiliano: 0759346439 au 0745114360
NYOTE MNAKARIBISHWA

WAHITIMU KIDATO CHA NNE 2019

Wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2019, wakiaga wadogo zao.



Share:

VERSE OF THE DAY - May 29. 2020

Isaiah 41:13

"For I, the Lord your God, hold your right hand; it is I who say to you, “Fear not, I am the one who helps you."

Share:

VERSE OF THE DAY - May 28, 2020

Share:

VERSE OF THE DAY - May 27, 2020


''Blessed are they that keep his testimonies,
and that seek him with the whole heart.''
Psalms 119:2 KJV


''Heri wazitiio shuhuda
zake, Wamtafutao kwa
moyo wote.''

Zaburi 119:2


Share:

VERSE OF THE DAY - May 26, 2020

''Greater love hath no man than this, that a man lay down his life for his friends.''

John 15:13 KJV
Share:

VERSE OF THE DAY - May 25, 2020

Luka 9:23-24

''23  Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.
24  Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.''
Share:

MUHUBIRI CHOIR - NENO LAKO (Busegwe Sec. SDA Church)

Share:

IBADA YA SHULE SABATO - 23 May, 2020 BUSEGWE SEC SDA CHURCH

Huduma ya SHULE SABATO sehuemu ya pili (23 May 2020) Iliendeshwa na MUHUBIRI CHOIR kwa njia ya mahojiano (kidijitali)..!

Mahojiano hayo yalifanyika kama taarifa ya habari na baadhi ya wanakwaya wakiwemo EMMANUEL WANDIBA(MTANGAZAJI), ELIHURUMA YESSAYA(UKUZIAJI), DICKSON MKAMA(UTUME) pamoja na Mwenyekiti wa kwaya Mwl. SYLIVESTER KAMALAMO aliyefanya mahojiano na Mch. GERALD NYAKIRERE wa mtaa wa Njiro (Rift Valley Field - ARUSHA)
Unaweza kuiskiliza moja kwa moja ama kuipakua kupitia blog hii hapa chini




Share:

VERSE OF THE DAY - May 24, 2020

Waebrania 12:11

''Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.''
Share:

VERSE OF THE DAY - May 23, 2020


Wagalatia 6:7


''Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.''

 
Share:

Juma la Tisa – Siku 100 za Maombi May 22 – May 28, 2020

KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO

UNIONI YA KASKAZINI MWA TANZANIA

CHAMA CHA WACHUNGAJI/HUDUMA ZA MAOMBI

SIKU 100 ZA MAOMBI:
MACHI 27 – JULAI 2, 2020


“Kumlilia Yesu wakati wa Uhitaji wetu mkuu!” 
Masomo haya yameandaliwa na Mark Finley ambaye ni Msaidizi wa Halmashauri Kuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato
Yametafsiriwa na Moseti Chacha na kuratibiwa na Huduma za Maombi NTUC.


Juma la Tisa – Siku 100 za Maombi May 22 – May 28, 2020

Wakati wa Kujichunguza MoyoNa Mark FinleyEe Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu; Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele..” – Zaburi 1 39:23:24

Miaka kadhaa iliyopita, mapema kabisa katika huduma yangu, niliitwa kuendesha juma la msisitizo wa kiroho kama Mkristo katika shule ya awali. Kadiri juma lilivyoendelea ilionekana wazi kwangu kuwa, walimu wawili walikuwa na mtafaruku mkubwa kati ya walimu wote waliokuwa pale. Mara nyingi tofauti zao zilifukuta hata kujitokeza katika mikutano ya walimu. Mmoja alipopendekeza wazo fulani, mwingine alilipinga. Nyakati ambazo wote walihudhuria kwenye mkutano wa waalimu, kulijitokeza mivutano isiyokuwa na maana. Ni dhahiri kwamba hakuna aliyekuwa akimpenda mwenzake kabisa.


Karibu na mwisho wa juma, nilihubiri kuhusu ombi kuu la upatanisho la Yesu katika sura ya 17 ya kitabu cha Yohana. Yesu alipokaribia kuachana na wanafunzi wake. Muda mfupi ujao angesalitiwa na kusulubiwa. Angefufuka kutoka kaburini na kupaa kwa Baba yake. Ombi lake la dhati liliakisi kile kilichokuwa ndani ya moyo wake. Ombi hilo lilidhihirisha kile kilichokuwa katika fikra zake kabla tu ya kifo chake pale msalabani. Mwokozi alikuwa akisumbuka kuhusu umoja wa kanisa. Aliomba kuwa, “Wote wawe na umoja; kama wewe Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.” (Yohana 1 7:21 ). Kristo alitamani kuwa mafarakano, wivu, kuhangaikia ukubwa, na migogoro kati ya
wanafunzi wake vyote vikome. Aliomba kwamba pamoja na tofauti zote hizo, umoja wao uoneshe uwezo wa upendo wake ulimwenguni.


Nilipokuwa nikiwashirikisha wanafunzi na waalimu jinsi moyo wa Kristo unavyotamani, jambo lisilo la kawaida lilitokea. Usiku wa mwisho wa juma hilo la msisitizo wa kiroho, tulipanga kuwa na huduma ya kuoshana miguu kisha meza ya Bwana. Roho Mtakatifu akaingilia kati. Mungu akawagusa kwa namna kuu. Wale waalimu wawili waliokuwa na mtafaruku walioshana miguu. Roho wa Mungu akavunja kuta za utengano. Wakakumbatiana, wakaungamiana mwenendo wao wa mtazamo hasi na hatimaye wakaomba pamoja.


Wanafunzi wa Yesu walipitia uzoefu kama huo, uliohusu toba na unyenyekevu katika zile siku 1 0 walipokuwa chumba cha juu ghorofani wakisubiri Pentekosti. Katika kipindi kile cha siku kumi, wanafunzi waliungamiana tofauti zao ndogo ndogo wao kwa wao. Walitubu wivu wao na kiburi chao. Mioyo yao ilijawa na upendo kwa Kristo ambaye alikuwa ametoa yote kwa ajili yao. Ni kwa namna gani walikuwa wakitamani kuwa wangeishi tena maisha kama haya miaka mitatu na nusu illiyopita.


Je, umeshawahi kujisikia hivyo? Umewahi kutamani kwamba ungerudisha mshale wa
saa ya maisha nyuma, ukarudi kutengeneza makosa ya zamani?


Tunapoona wema wa Mungu wenye upendo, na kutambua haki ya tabia yake, tunagundua udhaifu wetu, mapungufu, na dhambi zetu. Katika mng’ao wa nuru ya upendo wake usiokuwa na masharti pamoja na ukamilifu wake, mioyo yetu inanyenyekezwa. Tunaongozwa katika toba ya kina na maungamo. Tunamlilia apate kutuokoa na kutuhesabia haki ambayo ni yeye pekee anayeweza kutoa. Tunapozidiwa na ule utakatifu wake, tunaungana na nabii Isaya tukilia kwamba, “Ole wangu! Kwa
maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu…” (Isaya 6:5) Katika kujichunguza wenyewe tunamuuliza Mungu kuwa, “Je, kuna jambo lolote katika maisha yangu ambalo haliko sawa sawa na mapenzi yako?” Ndipo tunaomba kwa maneno haya: “Bwana nakuomba udhihirishe mwenendo ndani ya nafsi yangu ambao haufanani na Yesu.”


Lengo la Mungu katika mchakato wote huu ni kutuongoza karibu naye. Hahitaji watu kugaagaa katika hatia au kujazwa na majuto kwa maisha yetu yaliyopita. Lengo lake ni kutuongoza “katika njia ya milele.” Ingawaje ni jambo lenye ustawi kurudi na kutazama upya maisha yetu ya kiroho, hata hivyo siyo jambo lenye ustawi kudumu katika makosa ya maisha yetu yaliyopita. Kudumu katika makosa yetu yaliyopita na kujielekeza katika makosa hayo kwa kipindi kirefu kutaendelea kutukatisha tamaa tu.


Kumbuka kwamba siku zote Bwana wetu ni mkuu kuliko makosa yetu, na ni mkuu kuliko kushindwa kwetu. Ni dhahiri kwamba tunahitaji kufahamu hali yetu wazi wazi – lakini ni muhimu zaidi kufahamu neema Yake. Kuelewa udhaifu wetu kunatutayarisha kupokea nguvu zake. Kufahamu vyema hali yetu ya dhambi kunatutayarisha kupokea haki yake. Kuelewa vyema ujinga wetu kunatutayarisha kupokea hekima yake. Kusudi kubwa la ushawishi wa Roho ni kutuongoza kwa Yesu. Kadiri tunavyotambua dhambi zetu na makosa yetu kupitia katika mchakato wa kujichunguza au kujitathmini, tunaweza kumshukuru Mungu kwamba Roho wake Mtakatifu anatuongoza karibu ya Yesu, na kwa namna hiyo kutuvuta karibu sisi wenyewe kila mmoja kwa mwenzake. Ile nguvu ya Roho Mtakatifu inayoshawishi, inatutayarisha kupokea kwa ukamilifu Roho katika nguvu ya mvua ya masika. Lakini kabla Mungu hajatutengeneza, ni lazima atuvunje vunje. Kabla hajatujaza, ni lazima kwanza atufanye watupu. Kabla hajatuinua katika kiti cha enzi mioyoni mwetu, ni lazima aondoe kiburi kutoka katika mioyo yetu.


Mark Finley ni Msaidizi wa Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya kanisa la Waadventista
wa Sabato.


Maswali kwa Undani wa Moyo: Moyo wako leo uko wapi? Je, umewahi kupitia uzoefu wa zawadi tamu ya toba? Ikiwa ni hivyo je, unaona kama maisha yako yamebadilika kutoka katika hali uliyokuwa nayo hapo awali? Umepata uzoefu wa neema ya Mungu kwa namna iliyo mpya? Je, umejifunza kuendeleza neema hiyo kwa wengine?
Changamoto ya Moyo iliyo hai: Mwombe Mungu adhihirishie yale mambo yanayochukua muda wako katika maisha yako, mambo yanayoteka shauku yako, na yale yote yanayoondoa mivuto yako kutoka kwa Yesu. Kadiri unavyofikiria aya za Isaya
59:12 na 1 Yohana 1:9, omba na kumwambia Mungu adhihirishe nyufa zozote za kiroho ambazo zinaweza kuwa katika maisha yako. Omba kwamba aziondoe, na kukupatia hisia za kina za kujazwa na Roho Mtakatifu.

“Kutubu kunajumuisha huzuni kwa ajili ya dhambi, na kugeuka kwenda mbali nayo. Hatutaikataa dhambi mpaka hapo tutakapoona ubaya wake ulivyo hasa; yaani, hapatakuwa na badiliko la kweli katika maisha yetu mpaka hapo tutakapogeuka katika mioyo yetu na kwenda mbali nayo. Kuna watu wengi wanaoshindwa kuelewa jinsi kutubu kwenyewe kulivyo hasa. Wengi sana huhuzunika kwamba wametenda dhambi, na hata wanafanya matengenezo
ya nje, kwa sababu wanaogopa kwamba matendo yao mabaya waliyotenda yataleta
mateso juu yao wenyewe. Lakini huku si kutubu kwa maana ile ya Biblia. Wao huomboleza kwa ajili ya mateso wanayopata kuliko kwa ajili ya ile dhambi waliyotenda.
[Hayo yalikuwa ndiyo majuto ya Esau alipoona ya kwamba alikuwa ameupoteza urithi wake milele. Balaamu, alipotiwa hofu nyingi sana kwa ajili ya kumwona malaika aliyesimama mbele yake na upanga mkononi mwake, alikiri kosa lake asije akapoteza maisha yake; lakini hakutubu kwa kweli, nia yake haikugeuka, yaani, hakuchukizwa na yale maovu. Yuda Iskariote, baada ya kumsaliti Bwana wake, alisema, “Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia]…

Daudi aliuona ukubwa upitao kiasi wa kosa lake; aliona unajisi wa moyo wake; aliichukia
sana dhambi yake. Hakuomba ili apate msamaha tu, aliomba pia ili awe na moyo safi.
Alitamani sana kuwa na furaha iletwayo na utakatifu - yaani, kurejeshwa katika hali ya amani na ushirika na Mungu.”
Steps to Christ, uk. 23-25

Kuingia kwa undani – Mapendekezo ya Masomo ya ziada kwa Juma hili.
Ellen G. White,
Steps to Christ, sura ya 3, “Kutubu.”
Mark Finley,
10 Days in the Upper Room.Siku ya 57 – Kitovu cha Maombi – Ijumaa, 22 May 2020Taarifa za Sifa!
• Jinia Y.: “Ninamsifu Mungu kwa ajili ya Huduma ya vyombo vya Habari. Mahubiri
pamoja na shuhuda ambazo tunasikiliza na kutazama kwenye mitandao zimenisaidia kukabiliana na maumivu niliyokuwa nayo wakati huu wa kutengwa.”

• Yvonne L.: “Nilipata wito kupitia katika kazi yangu wa kumsaidia mtu fulani ambaye sikuwahi kukutana naye. Niliomba kwa ajli ya jambo hili, kisha nikaenda kumwona. Katika maongezi nikagundua kwamba mtu huyu alikuwa kiongozi katika kanisa la Waadventista wa Sabato aliyeacha Imani. Niliweza kuomba naye na akakiri kwamba amehisi Roho Mtakatifu akimwita arudi. Ninamsifu Mungu ambaye siyo kwamba anatoa tu fursa za kushuhudia tu, bali pia anatuonesha jinsi
ya kuitikia.”


MAMBO YA KUOMBEA
1. Ombea maeneo ambapo ugonjwa huu wa virusi vya corona unaonekana kuanza tena, kama vile Wuhan kule China na maeneo mengine ya miji na majimbo ya China.
2. Ombea waalimu wa Kiadventista katika shule zinazoendeshwa na serikali kule Thailand. Kuna uwezekano kwamba shule zitakapofunguliwa, serikali italazimisha masomo siku ya Jumamosi ili kufidia muda uliopotea. Omba kwa ajili ya kuimarika kwa Imani ya waalimu na kwamba wasimame imara kwa jinsi wale rafiki zake Danieli walivyosimama.
3. Ombea vikundi vidogo vidogo, makanisa ya nje, na mikutano ya kiinjilisti ambayo imeanzishwa kote katika Papua New Guinea kwa sababu ya kufungwa kwa makanisa.
4. Ombea huduma ya kanisa la Waadventista wa Sabato ya kituo cha Omega katika sehemu ya New Heaven, Connecticut kule Marekani, kinachohudumia watu wasiokuwa na makazi waweze kudumisha nafasi kwa kila mmoja ili kuepuka ugonjwa huu wa virusi vya corona.
 


Siku ya 58 – Kitovu cha Maombi – Jumamosi, 23 May 2020
 Umaskini Wenye Mibaraka
Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.” – Mathayo 5:3

“Wale wanaofahamu kwamba hawawezi kujiokoa wenyewe, au kutenda tendo lolote la
haki, hao ndio wanaofurahia msaada ambao Kristo anawapatia. Hao ndio maskini wa roho, ambao anawataja kuwa wenye heri. Hao ndio ambao Kristo amewasamehe, kwanza anawafanya watubu, na kazi hiyo ya kuwafanya hivyo ni kazi ya ofisi ya Roho Mtakatifu ambaye anawashawishi waone kwamba hakuna jambo jema ndani yao wenyewe. Wanaona kwamba kila jambo walilofanya limechanganyika na ubinafsi pamoja na dhambi. Kama yule mtoza ushuru aliyesimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, wanasimama mbali na kuijipiga-piga kifua wakisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi’ …Wale wote wenye hisia kwa kina za upungufu wao, wale wanaojisikia kwamba hawana kitu chema ndani yao, watapata haki na nguvu kwa kumtazama Yesu.” Thoughts from the Mount of Blessing, uk. 7-8

Maswali kwa Undani wa Moyo: Kujihesabia haki – Ile hali ya ndani ya kujisikia inayotundanganya tudhani kwamba tu wema – ni kikwazo kikubwa katika ukweli wa kupokea wokovu binafsi katika Yesu. Tunapotambua umaskini wetu kiroho, hitaji letu la dhati la Yesu, na kama matokeo ya kumwamini kikamilifu, kipindi baada ya kipindi, kwamba atatuponya kabisa kutoka katika mabaki ya ubinafsi, hapo ndipo tu tutakapokuwa na uhakika wa wokovu.
Kwa nini leo usije kwa Yesu jinsi ulivyo, pamoja na kiasi chochote ulichovunjika, hata na ubinafsi wenye dhambi? Kwa nini usidai tu damu yake, uhai wake, na kifo chake kama njia ya wokovu? Kwa nini usimuulize Yesu ang’oe ile hali ya kujiamini na kujitegemea ambayo bado imo ndani ya moyo wako, badala yake aweke Imani katika uwezo wake wa kukuokoa, na kukuwezesha kutenda kazi njema zinazohamasishwa na upendo usiokuwa na ubinafsi?


TAARIFA ZA SIFA:
• Nolubabalo D.: “Ahsante sana Bwana kwa mkono wako unaoonekana Afrika.
Ahsante sana kwa ulinzi wako. Ahsante sana kwa kuwalinda watoto wangu wakati nilipokuwa sipo. Unastahili kusifiwa.”
• Philippe M.: “Katika mji wetu wa Kananga hatukuwa na matangazo ya radio kabla ya kutangazwa kwa amri ya kubakia majumbani, lakini wakati huu wa janga hili tunavyo vituo vinne vinavyorusha matangazo kila juma kupitia katika radio nne mahalia. Tunamsifu Mungu kwa yote hayo!”
 

MAMBO YA KUOMBEA
1. Mwombe Yesu akusafishe kutokana na hali ya kujihesabi haki na akupatie kutambua kuwa kila siku na maisha yako yote unamhitaji Yeye sana.
2. Waombee wainjilisti kule Afrika Kusini ambao wanapambana na masuala mbalimbali ya kiafya na misongo. Omba kwamba waponywe na kuwezeshwa kupata namna ya kuhubiri injili pamoja na hali ilivyo.
3. Mwombee ndugu Samuel S. anayeumwa ugonjwa unaompa maumivu makali
katika sehemu chini ya mwili wake na madaktari hawajagundua tatizo linalomsibu. Mwombee pia dada Tabitha N. ambaye ameonekana kuwa na tundu kwenye moyo wake na anapitia kipindi cha maumivu makubwa. Ombea uponyaji wao na wengine wengi ambao wanaugua magonjwa mbalimbali wakati huu.

4. Ombea kituo cha Wizara cha China huko Jakarta, Indonesia kadiri wanavyoendesha mahubiri kwa njia ya mikutano ya mtandao kila Sabato kuanzia tarehe 9 May hadi tarehe 20 June 2020. Mkutano wa kwanza utawavuta watazamaji takribani 3000 na zaidi ya watu 260 wameshajisajiri kwa ajili ya
mafundisho ya Biblia



 

Siku ya 59 – Kitovu cha Maombi – Jumapili, 24 May 2020 
Huzuni ZimevunjwaHeri wenye huzuni; Maana hao watafarijika.” Mathayo 5:4

“Huzuni inayotajwa hapa ni huzuni ya moyo kwa ajili ya dhambi… Na kwa jinsi mtu anavyovutwa kumwangalia Yesu akiinuliwa msalabani, anatambua hali ya binadamu ya dhambi. Anaona kwamba ni dhambi ndizo zilimfanya Bwana wa utukufu akapigwa mijeledi na kusulubiwa. Anaona kwamba pamoja na kupendwa kwa upendo usiopimika, maisha yake yamekuwa ni mwendelezo wa uasi na ukosefu wa shukurani. Amemkataa yule aliyekuwa rafiki wake wa karibu na kuitukana zawadi ya thamani kutoka mbinguni. Amemsulubisha mwana wake wa pekee yeye mwenyewe na
kuuchoma upya ule moyo uliokuwa ukivuja kwa mapigo. Ametengwa na Mungu kwa ufa mkubwa wa dhambi ambao ni mpana na mweusi na wenye kina kirefu, na ana huzuni ya kuvunjika moyo. Huzuni ya jinsi hii itapata kufarijiwa. Mungu anadhihirisha hatia yetu ili tumkimbilie Kristo, na kupitia kwake tuwekwe huru kutoka katika kongwa la dhambi, na kufurahia katika uhuru wa mwana wa Mungu. Kwa majuto ya dhati tunaweza kuja chini ya msalaba, na hapo tukatua mizigo yetu.” Thoughts from theMount of Blessing, uk. 9-10,

Maswali kwa Undani wa Moyo: Umeshawahi kutenga muda wa kutafakari na kuona kile ambacho Yesu alitimiza kwa ajili yako katika saa ya giza ya kufa kwake? Kadiri unavyomwangalia, Mwokozi aliyesulubiwa, na kubeba dhambi, utaruhusu taswira ya matukio haya ipenye ndani ya moyo wako? Kadiri unavyozamisha kwenye fikra zako uzoefu wa maumivu yake kupitia katika kifo cha pili badala yako, utaruhusu hilo lifungue macho yako upate kuona jinsi dhambi unazopendelea zilivyo chafu mbele yake? Kwa nini leo usianze kuhuzunika kwa ajli ya dhambi zako, hasa kwa zile ambazo haukuwa tayari kuziacha? Ziungame kwa Yesu! Yeye atakusamehe kwa furaha kuu. Atakufariji, na atakupatia ushindi.

TAARIFA ZA SIFA:
• Diane T.: “Kumsifu Mungu kwa fursa ya kuhudhuria Kambi la Biblia kwa mtandao. Kumekuwa na mibaraka mingi wakati huu.”
• Iris R.: “Nilikuwa mraibu wa kuangalia Binge Netflix. Nilikuwa najaribu kusoma mistari kadhaa katika Biblia ili kujihalalisha, na kisha kuendelea kuangalia. Baada ya maombi ya juma moja shuleni kwetu Mungu alinionesha kwamba nahitaji kufuta program tumishi zinazohusiana na Binge Netflix. Baada ya muda nilirudi kuangalia filamu za Biblia, lakini sikuweza kujitawala, nilirudi tena katika utawala wa Shetani. Nilimlilia Mungu. Siku iliyofuata mchungaji alinipatia Biblia aina ya ‘Andrews Study Bible’ kama zawadi. Nilifurahi sana hadi machozi yalitiririka nikimshukuru Mungu kwa kuingilia kati.
Alinikumbusha aya ya Wafilipi 2:13 inayosema kuwa, “Kwa maana ndiye Mungu
atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi
lake jema.”
Ninamsifu Mungu kwa kunibadilisha na kunijaza ahadi zake.
 

MAMBO YA KUOMBEA
1. Omba kwa ajili ya uelewa dhahiri wa kile kilichotokea pale msalababi. Omba kwamba Mungu akusaidie kuchukia dhambi na kupenda haki.
2. Ombea kazi ya uuzaji wa vitabu kule Malawi pamoja na namna ya kuwategemeza kifedha ili waanzishe kituo cha uponyaji (sanitarium) na kazi za umisionari wa matibabu katika jimbo hilo.


3. Omba kwamba watu wasipelekeshwe na nadharia za njama, bali waelekeze macho yao kwa Yesu na katika ukweli wake.
4. Ombea washiriki wa kanisa la Waadventista wa Sabato wa Peter’s Rest katika visiwa vya Croix na Virgin. Jengo lao la kanisa liliungua na kuteketea kabisa. Omba kwamba wapate hekima ya namna ya kuanza upya na kuendelea ili hasara hii ibadilishwe na kuwa ushindi kwa Yesu.




 


Siku ya 60 – Kitovu cha Maombi – Jumatatu, 25 May 2020

Kuzawadia Unyenyekevu“Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.” Mathayo 5:5

“Asili ya binadamu siku zote inapambana kujitokeza, tayari kwa mahojiano, lakini yeye ajifunzaye kwa Kristo anaondolewa ubinafsi, kiburi, kupenda ubwana, na anakuwa na utulivu nafsini mwake. Ubinafsi unajiachia kwenye uwepo wa Roho Mtakatifu. Ndipo tunapopoteza shauku ya kutaka ukubwa. Tunakosa tamaa ya makuu ili kujitokeza tuonekane; lakini tunaona kuwa mahali petu pa juu sana ni miguuni pa Mwokozi. Tunamwangalia Yesu, tukisubiri mkono wake utuongoze, tukisikiliza sauti yake ituongoze.”
Thoughts from the Mount of Blessing, uk. 15

Maswali kwa Undani wa Moyo: Hakuna mahali penye furaha maishani kuliko kufahamu
kwamba unao upatanifu mkamilifu na Mungu katika mambo yote yale utendayo. Huu
upatanifu unakuwepo pale Yesu anapotafutwa, na ile hali ya kujikweza ikatupiliwa mbali,
ukitambua kwamba “Moyo (wenye dhambi) huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una
ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua”


(Yeremia 17:9). Unyenyekevu na upole wa moyo ni ufunguo wa kumruhusu Roho Mtakatifu kukuza ndani yako uzuri wa kweli, yaani tabia inayofanana na ya Kristo.
Je, utamuomba Yesu akuondolee tamaa ya kiburi na majivuno, tamaa ya kujiangalia kwa ubinafsi, na upendo wako wa ukuu? Utamwomba akuwezeshe kubadilisha hayo mambo kwa kukuwezesha kufanyia kai upole, unyenyekevu, na wema kuanzia leo?
 

TAARIFA ZA SIFA:
• Claudia P.: “Ninamsifu Mungu kwa rehema zake ambazo ni mpya siyo kila asubuhi tu bali wakati wote! Amekuwa mwema kwa familia yangu na mimi mwenyewe zaidi ya namna ambavyo maneno yanaweza kuelezea. Ninamsifu Bwana!”
• Rose K.: “Msifu Mungu kwa haya maombi ya siku 100! Kila siku ninasukumwa kufanya kitu kipya au kuona mabadiliko mapya kwa waumini wengine. Baadaye ninatambua kwamba kile nilichoona kwa kweli kilikuwa ni jibu kwa ombi fulani katika maombi haya ya siku 100. Ni jambo la kushangaza kuona jinsi Roho Mtakatifu anavyofanya kazi.”
 

MAMBO YA KUOMBEA
1. Omba kwamba Yesu akufanye mpole na mnyenyekevu
2. Ombea washiriki kule Uganda ambao wameathiriwa na mafuriko. Mafuriko yamesababisha nyumba nyingi kuanguka na kuharibika. Wengi hawana makazi na hasa kati ya hili janga ambalo katika nchi hiyo limesababisha kutokuruhusiwa kutoka majumbani mwao.
3. Omba kwa ajili ya waalimu Waadventista kote ulimwenguni wanapopitia katika ugumu wa kifedha kwa sababu ya kutokuweza kufanya kazi.
4. Omba kwa ajili ya vijana ili watambue umuhimu wa kumtumikia Mungu na siyo kuutumikia ulimwengu.



 


Siku ya 61 – Kitovu cha Maombi – Jumanne, 26 May 2020

Lishe ya Mwenye Haki“Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.” Mathayo 5:6

“Haki ni utakatifu, inafananishwa na Mungu, na ‘Mungu ni upendo’ 1 Yohana 4:16. Ni hali inayokubaliana na sheria ya Mungu, ‘… Maana maagizo yako yote ni ya haki’ (Zaburi 119:172) na ‘…pendo ndilo utimilifu wa sheria’ (Warumi 13:10). Haki ni Upendo, na upendo ni nuru na uzima wa Mungu. Haki ya Mungu imeunganishwa katika
Kristo. Tunapokea haki kwa kumpokea Yeye.” Thoughts from the Mount of Blessing, uk.18

Maswali kwa Undani wa Moyo: Je, una njaa na kiu ya haki ya Kristo? Maisha yake yenye upendo mkamilifu usiokuwa na ubinafsi, na kifo chake badala yetu kinakuwezesha
kupata zawadi mbili za neema iletayo haki:
1 . Kuhesabiwa haki, ambayo ni ahadi kwamba unafunikwa na maisha yake makamilifu kupitia katika Imani kwenye hiyo ahadi.
2. Kupewa haki, ambayo ni ahadi kwamba atakubadilisha kutoka katika kuwa mwenye ubinafsi hadi kuwa kiumbe unayeakisi upendo wa Yesu usiokuwa na ubinafsi, kupitia katika Imani hai kwenye hiyo ahadi
Zawadi mbili hizi zitakukamilisha, zitakushibisha kwa hakika, zitakuokoa! Kwa nini
usizikubali leo hii na kuanza kuishi maisha mapya ya furaha yaliyojawa na Yesu katika
kutambua uhalisia wake unaoshangaza wa upendo wa Mungu ukomboao?
 

TAARIFA ZA SIFA:
• Jane D.: “Mungu amemponya mgonjwa niliyekuwa nikimwombea. Na kwa namna ya ajabu amegusa mioyo ya familia yangu.”
• Marcia N.: “Binti yangu amekuwa mraibu wa madawa ya kulevya kwa miaka mingi, ameishi bila makao, na hata akapelekwa gerezani. Vikundi vyetu vya maombi vilianza kumwombea na matokeo yake amefanikiwa kujiunga na kitengo kinachosaidia waathirika wa jinsi hii akipata msaada, na afya yake inaendelea vizuri, ameanza kuwa na shauku kwa mambo ya Mungu na anasoma vitabu vya
Roho ya Unabii. Anasema kuwa ni Mungu aliyemsaidia. Ninamsifu Mungu kwa upendo wake kwetu na jinsi alivyotusaidia katika kipindi chote cha hii miaka ya kuvunjika moyo” Vilio vinaendelea usiku, lakini furaha huja asubuhi.
 

MAMBO YA KUOMBEA
1 . Omba kwamba haki ya Kristo ikufunike na kukujaza.
2. Omba kwamba Mungu aingilie kati katika mlipuko wa ugonjwa wa uti wa mgongo katika jimbo mojawapo huko Ghana. Mlipuko huu tayari umeshaua watu wengi katika jimbo hilo.
3. Ombea makanisa ambayo hayajishughulishi tangu ugonjwa huu wa virusi vya corona ulipolipuka. Ombea wachungaji, viongozi wa kanisa, na washiriki wapate kufahamu namna bora ya kujiunganisha wakati huu. Omba kwa ajili ya mtazamo mpya kuhusu umuhimu wa maombi.
4. Ombea washiriki wa Myanmar kadiri wanavyojaribu kutumia mitandao kueneza
injili wakati huu wa zahama

. 

Siku ya 62 – Kitovu cha Maombi – Jumatano, 27 May 2020 
Uwe na Rehema!Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema. Mathayo 5:7

“Mungu mwenyewe ni chanzo cha rehema yote. Jina lake ni
‘…mwingi wa huruma,mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli’ Kutoka 34:6. Hashughuliki na sisi kwa namna tunayostahili. Wala haulizi kama tnastahili upendo wake, bali anamimina juu yetu utajiri wa upendo wake, ili kutufanya tustahili. Siye mwenye kulipiza kisasi. Hatafuti kuadhibu bali kukomboa… Anatamani sana kuwaondolea wanadamu adha na masumbufu yote, kuweka dawa kwenye vidonda vyake… Wenye rehema ni warithi wa asili ya kimbingu, na ndani yao ule upendo wa Mungu ulio na huruma unajidhihirisha. Wale wote wenye mioyo yenye huruma na upendo wa milele, watatafuta kuokoa wala siyo kushutumu. Uwepo wa Kristo katika nafsi zao ni chemchemi isiyokauka. Pale alipo, kutakuwa na bubujiko la wema.” Thoughts from the Mount of Blessing, uk. 22

Maswali kwa Undani wa Moyo: Chukua muda kutafakari kuhusu rehema za Mungu katika maisha yako. Anakutakika mema, bila kujali ukosefu wa uaminifu wako. Hahitaji uhakikishe kwamba unastahili ili kupokea zawadi yake ya wokovu. Anakuchukulia kwa upendo. Unapopitia katika uzoefu wa ndani wa rehema za Mungu, Roho Mtakatifu atakuwezesha kuwa wakala wa rehema; ukishughulika na wale wanaokuzunguka kwa
upendo huo huo na rehema. Hasa wale ambao wamekukosea. Je, leo hii utachagua kwa msaada ya Yesu kuendeleza rehema za Mungu kwa watu
walio katika maisha yako? Kuwasamehe kabla hawajaomba msamaha, kuwapenda kabla haujapewa sababu ya kufanya hivyo? Kuwatakia mema bila kujali kama wanastahili au la?


TAARIFA ZA SIFA:
• Elham L.: “Nimekuwa nikiomba niwe na uhusiano wa kina na Mungu. Tangu nilipojiunga na mpango wa maombi ya siku 1 00 kila siku katika ibada zangu za asubuhi nikitumia mtiririko wa jinsi ya kuomba, maisha yangu yamehuishwa. Umekuwa ni mlipuko ambao sikutazamia.
• Sherma J.: “Mungu amejibu maombi kwa mshiriki aliyepotea. Alipuuza jitihada zangu za kumwita. Nilipomtembelea, aliongelea tu kuhusu matatizo yake bila kunipa nafasi ya kuzungumza. Nilimwomba Mungu afanye kazi ndani ya moyo wake kwamba, badala ya mimi kumwita, yeye ndiye aniite. Majuma mawili baadaye aliniita na kusema kwamba matatizo yake yameisha na kwamba alitaka kurudi kanisani na kutoa maisha yake upya kwa Mungu!”
 

MAMBO YA KUOMBEA
1 . Mwombe Mungu akufanye kuwa wakala wa rehema zake kwa watu walioko katika maisha yako.
2. Ombea wanafunzi ambao wanahangaika kupata karo za shule ili waendelee na elimu. Omba kwamba wawezeshwe kupitia uzoefu wa uongozi wa Mungu katika elimu yao.
3. Omba kwa ajli ya watu na washiriki wa Zimbabwe. Wengi wao hawawezi kumudu kubaki majumbani mwao kulingana na amri ya kutokutoka nyumbani. Mfumo wa huduma za afya hauwezi kushughulika na janga hili la maambukizi ya virusi vya corona.
4. Ombea wachungaji kadhaa kule Indonesia walioambukizwa na ugonjwa wa corona.
5. Omba kwamba Mungu abariki mpango wa wanafunzi wa kutoka na kuwafikia watu kule Brazil unaofanyika kwa kujitolea kuzalisha vitakasa mikono kwa ajli ya wazee.



 
Siku ya 63 – Kitovu cha Maombi – Alhamisi, 28 May 2020 
Maono SafiHeri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. Mathayo 5:8

“Roho Mtakatifu anachukua ukweli kumhusu Mungu pamoja na mwengine yeyote yule aliyemtuma, na kuuleta katika uelewa wa ndani ya moyo. Wenye moyo safi wanamwona Mungu katika uhusiano mpya ulio mzuri, kama Mkombozi wao, na wakati wakitafakari tabia yake iliyo safi na yenye upendo, wanatamani kuakisi sura yake. Wanamwona kama Baba mwenye shauku ya kumkumbatia mwana aliyetubu, na mioyo yao inajazwa na furaha isiyoelezeka yenye utukufu mkamilifu.”
Thoughts from the Mount of Blessing, uk. 26

Maswali kwa Undani wa Moyo: Tunapotembea na Mungu kwa uaminifu, anaendelea kufungua macho yetu kwa uelewa zaidi na zaidi wa tabia yake ya upendo, nia yake, na uzuri wake. Katika kutambua utakatifu wake ulio mkamilifu, na usafi wake, uchafu wetu unadhihirika na tunakaribishwa kupokea utakaso ambao ni yeye pekee awezaye kuutoa. Upande huu wa mbingu tunaona kwa macho ya Imani, lakini siku moja hivi karibuni, tutamwona uso kwa uso! Hiyo itakuwa ni siku ya utukufu. Hadi hapo, kwa nini usimwombe ausafishe moyo wako kutoka katika uchafu na uovu? Kwa nini usitafute kwa dhati maono dhahiri na uelewa kutoka kwa Mungu na nia yake?


TAARIFA ZA SIFA:

• Shana S.: “Katika kipindi hiki cha Maombi ya siku 1 00 nilianza kumwombea rafiki yangu wa miaka 20 ambaye bila sababu yoyote alianza kunipuuza kuanzia mwaka 201 7. Akanifungia kwenye simu yake na mengine mengi. Nilijaribu mara kadhaa kumfikia lakini hakuitika. Kiongozi wetu wa maombi alituhimiza kumlilia Mungu. Mimi nilifanya hivyo, nikaita tena lakini hapakuwa na jibu lolote. Siku iliyofuata aliniita! Alifungua simu yake kwamba sasa naweza kumpigia na akaniambia kwamba sikuwa nimetenda jambo lolote baya. Tukarudi kuunganika tena na kupatana. Mungu alijibu maombi yetu.”


• John K.: “Huku Uganda amri ya kutokutoka nyumbani imesababisha njaa kwa watu wengi. Katika kipindi cha maombi haya ya siku 1 00 Mungu amenipatia hekima ya kuwasaidia watoto wenye njaa. Nilipeleka ujumbe kwa familia 1 00 kutoka kanisani na kuwaomba washiriki kuchangia vyakula kwa ajli ya watu wenye njaa jirani yangu. Wazo hili la kawaida tu lilisambaa kote katika jimbo kupitia kwa waandishi wa habari walioliweka mtandaoni. Kwa kuunganishwa upya sasa tumeanza muunganiko wa WhatsApp tukijenga katika mikutano ya uinjilisti!”

MAMBO YA KUOMBEA
1 . Omba kwa ajili ya moyo safi, uhuru kutoka katika dhambi, kusafishwa kutoka katika kila aina ya uchafu.
2. Ombea wakurugenzi wanaohusika na mazishi, wahudumu wa vyumba vya maiti, na wafanyakazi wote wanaohusika na huduma za mazishi kadiri wanavyohusika moja kwa moja wakigusana na wengi waliokufa kwa ugonjwa huu unaoambukizwa na virusi vya corona.
3. Ombea kanisa kule Fiji, kadiri wanavyofikiria kubadilisha muundo, kwa kuimarisha na kuwezesha walei kumiliki majukumu mbalimbali.
4. Omba kwa ajili ya huduma ya kanisa la Waadventista wa Sabato la ‘Harvest’ kule Alabama, Marekani. Hawa wako katika maeneo ya kipato cha chini, maeneo yenye vitendo vingi vya jinai, na watu wachache wanoongoka kwa jitihada za kuongoa roho. Waombee kwamba Mungu alete namna ya kujikwamua.
Share:

VERSE OF THE DAY - May 22, 2020

John 14:1 KJV

''Let not your heart be troubled: ye believe in God, believe also in me.''
Share:

VERSE OF THE DAY - May 21, 2020

Revelation 3:20

''Behold, I stand at the door, and knock: if any man hear my voice, and open the door, I will come in to him, and will sup with him, and he with me.''

 ''Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami''

Ufunuo 3:20

Share:

VERSE OF THE DAY - MAY 20, 2020

''He that believeth on him is not condemned: but he that believeth not is condemned already, because he hath not believed in the name of the only begotten Son of God.''
John 3:18 KJV
Share:

kumbukizi May 16, 2020






















Share:

VERSE OF THE DAY - May 19, 2020

Isaya 26:3

''Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.''
Share:

IBADA YA SABATO TAKATIFU - May 16, 2020 by Mwl. ELIHURUMA YESSAYA MMBAGA


IBADA YA SABATO TAKATIFU 16/05/2020

MNENAJI MKUU: 
Mwl. ELIHURUMA YESSAYA MMBAGA  

FUNGU KUU: ZEKARIA 9:11-12

WIMBO MKUU (Nyimbo za kristo);
NO 119 Alilipa bei  

KWAYA(WIMBO):HEBU NENDA HOSPITALINI
 
                SOMO; KUIRUDIA NGOME.

Ø   Ananukuhu kitabu cha Zekaria 9;11-12 (Irudieni ngome enyi wafungwa wa tumaini)
Wito wa biblia katika dunia ya leo ni kuirudia Ngome.

Je ngome ni nini?
Ngome ni eneo/jengo kubwa lililoimarishwa kwa silaha za kivita kwa ajili ya kujihami na maadui (Kamusi ya Kiswahili) .Hii ilifanyika saana nyakati za zamani, mfano taifa la Israel na maadui zao tofauti na sasa. Ilisadikika ndipo penye usalama pekee wakati wa vita.Miji mingi ilizungushiwa ngome kwa kutumia kuta zilizo imara. Ilimpasa adui avunje kwanza ngome ya mji huo ndipo aweze kuwafikia mateka wa eneo hilo na bila kuvunja ngome huwezi kufanikiwa katika uvamizi huo na kupata mateka.
 
Mtunga ZABURI 27;1-2 anasema (Bwana ni ngome yangu nimhofu nani?) anasema pia BWANA ni  NGOME ya uzima.shetani hawezi kutuweka mateka kama BWANA ndiye ngome yetu.

Kisa cha mtu mmoja aliyeiacha ngome
Mtu huyu alikuwa katika ngome akaiacha na baadaye akairudia ngome. Je wajua ni nani na  ni  kwa vipi aliirudia ngome?.Ambatana nami asubuhi ya leo.

Ø  Ngome kamwe haiwezi kukuacha bali wewe ndiye waweza kuiacha ngome.mfano, Mungu hawez kutuacha bali sisi ndio twaweza kumuacha Mungu.
Kitabu cha Waamuzi 13;16 kinaeleza ujio wa Samsoni  mnadhiri wa MUNGU na uwepo wa wazazi wake. Wazazi  wa Samson wanapewa maelekezo namna ya kumlea mototo huyu (Samson).
Samson alipoiacha ngome maadui walipata nafasi ya kumfanya yeye mateka.
Kejeli dhidi ya shujaa huyu wa Mungu zilimfanya samsoni aonekane kuwa yeye si kitu kabisa.
Walifanikiwa kufungua mlango wa ngome ya Samsoni kwa kutumia Delila(mke wa samsoni) kisha kumtoboa macho.

Upofu wa macho ya Samsoni ulimfanya afungue macho ya kiroho hata akarudishiwa nguvu za kuwaangamiza wafiristi.
Ili uweze kufumbuliwa macho ya kiroho kubali kutobolewa macho ya kimwili kwanza.
Samsoni anafanikiwa kuirudia ngome.alipokuwa amekamatwa na kuwekwa mbele ya wafiristi katika jengo la maonesho,kama mfanya maonesho. Samsoni alijihisi kama kiongozi mkuu wa wenye dhambi.
Nakupendekezea leo umpende (na kuwa kama) Samsoni aliyetobolewa macho na si Samsoni asiyetobolewa macho
Kwa nini nakupendekezea samsoni aliye tobolewa macho?
Kwa sababu ya upofu  wa macho yake samsoni anaanza kuwa;
·         Mnyenyekevu.
·         Mwenye maombi mengi.
·         Mwenye Kumtafuta Mungu.
·         Anajiona mwenye mapungufu makubwa sana.
·         Alimtafuta Mungu katika nyakati za kujiliwa kwake.
Samsoni anatumika kama kiburudisho mbele ya miungu ya wafilisti(dagon) na kelele za dhihaka za wafilisti kwa samsoni ziliibua hisia za kumtafuta Mungu ndani ya moyo wake na shetani alitumia nafasi hii kupitia wafilisti kwa kumzomea na kuonyesha kuwa yeye(Samsoni) si kitu. Lakini Samsoni alisema moyoni mwake KRISTO ni vyote kwangu na akiwepo yeye ni salama rohoni. 

Waamuzi 16;28 (Samsoni anamwita BWANA)Bwana niokoe kwa wakati huu tu..
Wakati mwingine tunazama dhambini na tunapohitaji kutubu shetani anatukumbusha dhambi zetu na tunashindwa kumrudia Mungu wetu.Lakini kwa Samsoni hakujali,Alimwita Bwana na kuomba nguvu yake kwa wakati mchache tuu.
Kama kwa samsoni, AMINI SASA UMESAMEHEWA usiogope Mrudie Mungu naye yuko tayari kukupokea.
Wito wangu kwako leo ni kwamba kila mtu na airudie ngome (Zaburi 27;1)
Nitakapo simama miguuni pa Yesu taji nitaweka miguuni pake
MUNGU   AWABARIKI

Kutazama ibada hii bofya hapa pia usisahau ku'like na ku'subscribe katika YOUTUBE channel yetu ili uweze kupata updates mbalimbali na kubarikiwa.

Pia waweza kutazama video hii hapa chini
Share:

Translate

Categories

USOMAJI WA BIBLIA KWA MPANGO

...

BUSEGWE GIRLS HIGH SCHOOL

Tunapokea wanafunzi Kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 2021 kuanzia tarehe 7 Januari.
Pia nafasi za wahamiaji kidato cha tano zipo!
NYOTE MNAKARIBISHWA
Mawasiliano: +255759346439 (Mkuu wa Shule)
+255745114360 (Mhazini)

Support

Kanisa letu ni kanisa la shule ya sekondari ya wasichana Busegwe, katika jimbo la Mara. Shule hii ina uhitaji mkubwa wa kifedha kwa ajili ya maendeleo. Hivyo, kwa unyenyekevu, tunasihi sapoti yako ilikuweza kuiendeleza na kufanikisha programu mbalimbali ikiwemo uinjilisti.

Wasiliana nasi kwa mawasiliano yaliyo tolewa hapo chini au bofya HAPA