BUSEGWE GIRLS' HIGH SCHOOL

Tunapokea wanafunzi Kidato cha kwanza hadi cha nne kuanzia tarehe 7/1/2021 Pia nafasi za wahamiaji kidato cha tano zipo!
Mawasiliano: 0759346439 au 0745114360
NYOTE MNAKARIBISHWA

DAILY DEVOTIONAL - The Spirit Must Illuminate the Word

We have received, not the spirit of the world, but the Spirit who is from God, that we might know the things that have been freely given to us by God.
1 Corinthians 2:12, NKJV.


Share:

VERSE OF THE DAY - July 30, 2020


Know ye not that ye are the temple of God, and that the Spirit of God dwelleth in you?
1 Corinthians 3:16 KJV
Share:

AFYA YETU - FAHAMU FAIDA ZA PARACHICHI (AVOCADO) KWA MAMA MJAMZITO

PARACHICHI ni miongoni mwa tunda zuri sana kwa mama mjamzito kwa sababu lina wingi wa madini ya pottasium, folate, vitamins C, E, & B6 ambazo huimarisha utengenezaji wa ubongo na mfumo wa fahamu wa mtoto kwa ujumla.
Vilevile husaidia sana katika kumkinga mtoto dhidi ya hatari ya kuzaliwa na tatizo la mgongo wazi (Meningocele).
Aidha kwa mama mjamzito husaidia kuimarisha Kinga ya mwili wake kutunza ujauzito huo pamoja na changamoto ya kuugua magonjwa ya mara kwa mara, kwa kipekee kabisa hupunguza tatizo na kuwashwa pamoja na kuvimba miguu hasa kwenye hatua ya tatu ya ujauzito (Third Trimester).
Share:

VERSE OF THE DAY - July 29, 2020


And the light shineth in darkness; and the darkness comprehended it not.
John 1:5 KJV
Share:

VERSE OF THE DAY - July 28, 2020


Proverbs 4:23 NIV

Above all else, guard your heart, for everything you do flows from it.
Share:

WE WISHES YOU HAPPY SABBATH - July 25, 2020



Share:

VERSE OF THE DAY - July 24, 2020


Yet if any man suffer as a Christian, let him not be ashamed; but let him glorify God on this behalf.
1 Peter 4:16 KJV
Share:

AFYA YETU - FAHAMU MAGONJWA YANAYOSABABISHA KUZIBA KWA MRIJA WA MKOJO (URETHRAL STRICTURE)

Mrija wa mkojo (urethra) ni njia ya kutolea mkojo nje ya mwili kutoka kwenye kibofu na unapoziba hufanya utokaji wa mkojo kuwa wa tabu na kusababisha maumivu makali sana. Kitaalamu kuziba kwa mrija wa mkojo huitwa urethral stricture na husababishwa na kovu linalotokea katika sehemu ya mrija baada ya mtu kuumia, kufanyiwa upasuaji au kupona magonjwa ya zinaa.
Magonjwa ya zinaa yanayoweza kusababisha kovu kwenye njia ya mkojo yapo mengi na tutayajadili katika matoleo yetu yajayo kwani  yapo mengi.

Hivyo ni muhimu sana mtu kutibiwa mapema anapokuwa na magonjwa hayo.
Kuziba kwa mrija huo kunaweza pia kusababishwa na uvimbe karibu na eneo la kinena unaokandamiza mrija.

Wengi wanaopatwa na tatizo hili ni wale ambao wana historia ya kuugua magonjwa ya zinaa au kuwahi kuwekewa mipira ya mkojo au vifaa vya namna hiyo (catheter au cystoscope) sehemu hizo au husababishwa na kuvimba tezi dume (BPH) kwa wanaume.
Wengine wanaopatwa na tatizo hili ni wale wanaokuwa na historia ya kuumia au kupata majeraha maeneo ya sehemu za siri au  wanaopata maambukizi ya mara kwa mara ya magonjwa kwenye mrija wa mkojo (urethritis).
Tatizo hili mara nyingi huwakumba wanaume na ni mara chache sana kuwakumba wanawake au watoto wachanga  labda wale wanaozaliwa wakiwa na tatizo hili ambapo kitaalamu huitwa congenital urethral stricture.

DALILI.

Mtu mwenye tatizo hili anaweza kuwa na dalili zifuatazo:

⏺kwa mwanaume hutokwa na manii zilizochanganyika na damu.

 ⏺kukojoa mkojo mweusi au uliochanganyika na damu,

⏺kutoa mkojo kidogo sana tena kwa shida, kukojoa mara kwa mara na kushindwa kumaliza mkojo wote.

⏺Wengine huona dalili za mkojo kujitokea wenyewe, hivyo mhusika kujikojolea, kusikia maumivu wakati wa kukojoa au chini ya tumbo au kwenye kinena,  mkojo kutawanyika ovyo wakati wa kukojoa na uume kuvimba.
Mgonjwa aonapo dalili hizo anashauriwa kumuona daktari  ili afanyiwe uchunguzi wa mwili na namna anavyokojoa. Uchunguzi wa mwili unaweza kuonesha kupungua kwa mkondo wa mkojo, uchafu kutoka katika mrija wa mkojo, kibofu kilichojaa/kuvimba kwa mitoki ya maeneo ya kinena, tezi dume iliyovimba au yenye maumivu, kuhisi kitu kigumu chini ya uume.
Daktari akiona moja ya dalili hizo mgonjwa anaweza kuchunguzwa kwa vipimo tofauti kama vile kile cha kuchunguza mrija pamoja na kibofu cha mkojo (cystoscopy),kuangalia kiasi cha mkojo kinachobaki katika kibofu baada ya mkojo kutoka, X-ray ya mrija wa mkojo (Retrograde urethrogram) atapimwa kama ana magonjwa ya zinaa kwa kumfanyia uchunguzi wa mkojo (Urinalysis) pamoja na kuotesha mkojo (Urine culture).

USHAURI.

⏺Mgonjwa mwenye tatizo hili atibiwe haraka maana kama tatizo likiachwa linaweza kusababisha kuziba kabisa kwa njia ya mkojo na kusababisha mkojo kujaa katika kibofu, hali ambayo, pamoja na kuleta maumivu makali kwa mgonjwa inaweza pia kusababisha figo kushindwa kufanya kazi.

⏺Watu wajikinge na magonjwa ya zinaa ambayo yanasababisha tatizo hili na wawe  makini na kazik zinazoweza kusababisha kuumia sehemu nyeti na kuzalisha tatizo hili.

Share na mwenzako apate elimu hii pia.
Share:

VERSE OF THE DAY - July 22, 2020


Finally, brethren, whatsoever things are true, whatsoever things are honest, whatsoever things are just, whatsoever things are pure, whatsoever things are lovely, whatsoever things are of good report; if there be any virtue, and if there be any praise, think on these things.
Philippians 4:8 KJV
Share:

VERSE OF THE DAY - July 19, 2020


Casting down imaginations, and every high thing that exalteth itself against the knowledge of God, and bringing into captivity every thought to the obedience of Christ;
2 Corinthians 10:5 KJV
Share:

WE WISHES YOU HAPPY SABBATH - July 18, 2020


Sabato njema sana!
Share:

AFYA YETU *IJUE SARATANI YA MATITI (BREAST CANCER )*

Saratani ni aina ya ugonjwa unaosababisha ukuaji wa seli za mwili kubadilika na kukua bila mpangilio maalum.

Saratani ya matiti hutokea kwenye titi ambalo kwa kawaida lina sehemu ya kutengeneza maziwa ijulikanayo kama lobules na aina fulani ya mishipa inayounganisha hizi lobules na chuchu za titi. Sehemu kubwa iliyobakia ya matiti inajumuisha mafuta na tishu ambazo kitaalamu tunazoita connective and lymphatic tissue. Saratani ya matiti inayotokea kwenye lobules huitwa lobular carcinoma na ile inayotokea kwenye ducts huitwa ductal carcinoma.

Baadhi ya saratani ya matiti zinaongeza ukubwa kutokana na kuwa na vishikizi aina ya receptors zinazojulikana kama estrogen receptors kwenye seli zao ambazo husababisha ukuaji wa saratani ya matiti.

Kuna wanawake wengine wana viashiria vya asili vinajulikana kama HER2 positive breast cancer ambacho husaidia seli kuongezeka, kugawanyika na kujirekebisha pale zinapoharibika. Kiashiria hiki kinaaminika ndicho kinachosababisha wanawake hawa kuwa na saratani ya matiti yenye madhara zaidi na kuwa na uwezekano mkubwa wa kujirudia kwa saratani baada ya tiba tofauti na wale ambao hawana kiashiria hiki cha HRE2.

Vihatarishi vya Saratani
Kuna mambo kadhaa ambayo yameonekana kuwa na uhusiano, ama wa moja kwa moja au kwa kupitia vitu vingine, wa kusababisha saratani ya matiti, au kumfanya mtu au kundi la watu kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa huu kuliko wengine. Mambo hayo ni pamoja na

Jinsia: Ingawa, saratani ya matiti huweza kutokea kwa wote wanawake na wanaume, imeonekana kuwa wanawake ni waathirika wakubwa zaidi wa saratani hii ikilinganishwa na wanaume.
👉Umri: Uwezekano wa kupata saratani hii huendana na umri wa mtu. Kadiri umri wa mtu unavyoongezeka ndivyo pia uwezekano wa kupata saratani hii unavyozidi kuwa mkubwa. Wanawake walio na umri wa kuanzia miaka 50 wapo kwenye hatari kubwa (mara 2 au 3 zaidi) kuliko walio na umri wa miaka 45.
Uasili wa mtu (ethnicity): Saratani ya matiti hutokea zaidi kwa wanawake wazungu kuliko wanawake wa kiafrika au wenye asili ya afrika (weusi).

👉Uzazi: Wanawake ambao hawajazaa au kunyonyesha wapo kwenye hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti. Wanawake wanaopata ujauzito kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 nao pia wapo kwenye hatari kubwa ya kupata saratani hii.
Historia ya ugonjwa huu katika familia: Wanawake walio katika familia zenye historia ya ugonjwa huu wana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya matiti ukilinganisha na wale ambao hawana historia ya ugonjwa huu katika familia zao. Kwa mwanamke aliye na ndugu (mama, dada au mtoto) ambaye aliwahi kupata saratani hii kabla ya umri wa miaka 50, uwezekano wa mwanamke huyu kupata ugonjwa huu ni mara mbili ya yule ambaye hana historia hii.
👉Umri wa kuvunja ungo: Wanawake wanaovunja ungo (kupata hedhi) kabla ya umri wa miaka 12 wapo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu.
Kuacha kupata hedhi: Kwa kawaida wanawake huacha kupata hedhi wafikapo miaka 45, hali ambayo kitaalamu hujulikana kama menopause. Wanawake wanaochelewa kuacha kupata hedhi, kwa mfano wale wanaoendelea kupata hedhi wakiwa na zaidi ya miaka 45, wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata saratani ya matiti.
👉Historia ya saratani ya matiti: Wanawake ambao wamewahi kupata ugonjwa huu kwenye titi la upande mmoja hapo kabla, wana uwezekano mkubwa wa kupata tena saratani kwenye titi la upande mwingine hapo siku za usoni.
👉Ulaji wa vyakula venye mafuta mengi: Tafiti zinaonesha kuwa, wanawake wanaopendelea kula vyakula vyenye mafuta mengi wapo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu.
Kuongezeka uzito: Tafiti nyingine zimeonesha kuwa, wanawake wanene wana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya matiti ukilinganisha na wale wa uzito mdogo au wa kati.
👉Uvutaji sigara: Kuna matokeo yenye kukinzana kuhusu uhusiano wa uvutaji sigara na hatari ya kupata saratani ya matiti. Wakati baadhi ya tafiti zinaonesha uhusiano wa karibu kati ya uvutaji sigara na uwezekano wa kupata saratani ya matiti, tafiti nyingine zinaonesha majibu yenye kutofautiana kuhusu uhusiano wa uvutaji wa sigara na saratani ya matiti. Hata hivyo, kwa ujumla, wanawake wanaojizuia kuvuta sigara wanakuwa na afya njema zaidi kuliko wale wanaovuta sigara.
👉Unywaji pombe: Imeonekana kuwa wanawake wanaokunywa pombe zaidi ya chupa moja kwa siku wana uwezekano wa kupata saratani ya matiti kwa asilimia zaidi ya ishirini.
Historia ya tiba ya mionzi: Wanawake ambao wamewahi kupata tiba ya mionzi hususani wakati wa ukuaji wa matiti, wapo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu. Hali hii husababishwa na ukweli kuwa mojawapo ya madhara ya mionzi ni kuongeza uwezekano wa kupata saratani ya aina yoyote.
👉Matumizi ya dawa za kupanga uzazi: Kuna ushahidi kuwa saratani ya matiti ina uhusiano na matumizi ya muda mrefu ya vidonge vya kupanga uzazi.
Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni mwilini: Kwa wale wanaotumia tiba ya homoni inayojulikana kama hormone replacement therapy, kwa sababu nyingine yeyote ile, au wale wenye kiwango kikubwa cha homoni kama vile oestrogen na progesterone mwilini mwao wapo kwenye hatari zaidi ya kuugua saratani ya matiti.
👉Kuwa na matiti makubwa: Wanawake wenye matiti makubwa (dense breast tissue) wana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya matiti. Hali hii hutokana na ukweli kuwa wakati mwingine ni vigumu sana kwa madaktari kutambua kama wana saratani au la kutokana na ukubwa wa matiti yao.
Saratani husambaa vipi?
Kwa kawaida saratani husambaa kwa njia tatu zifuatazo

👉Kupitia tishu - Saratani husambaa kwenye tishu za kawaida ambazo zimezunguka eneo la saratani.
Kupitia mfumo wa limfu (lymphatic system) - Saratani huvamia mfumo wa lymph na kufuata mishipa yake hadi sehemu nyingine za mwili.
👉Kupitia damu - Saratani inaweza kusambaa kupitia damu kwa kuvamia mishipa ya damu ya vena na capillaries (veins and capillaries) na kusafiri kutumia damu hadi sehemu nyingine za mwili.
Dalili za Saratani ya Matiti
👉Dalili ya awali inayoweza kutambulisha saratani ya matiti ni kuwepo kwa uvimbe kwenye titi ambao huwa na hali tofauti na sehemu nyingine za titi. Hata hivyo, si kila uvimbe kwenye titi unaashiria uwepo wa saratani ya matiti. Uvimbe huu huwa mgumu, unaochezacheza kwenye titi, ambapo wakati mwingine unaweza kuwa na maumivu makali au kusiwe na maumivu yeyote. Uvimbe huu huwepo zaidi ya mzunguko mmoja wa hedhi kwa wale ambao hawajaacha kupata hedhi.

👉Dalili nyingine ni pamoja na
Kuwepo kwa uvimbe kwenye sehemu za kwapa

Sehemu ya titi kuingia ndani inayoashiria uvimbe usioonekana au usioweza kuhisiwa
Mabadiliko kwenye chuchu, kama vile chuchu kuzama ndani au kuwa na nundu ndogo ndogo, chuchu kuwasha, kuhisi kama kuchoma, kidonda kwenye chuchu au chuchu kuwa na kovu ambalo huashiria saratani ya sehemu hiyo
👉Kubadilika kwa umbo la titi, ngozi ya titi kuwa kama ganda la chungwa (peu de orange), ngozi kuwa na rangi nyekundu, na kuongezeka kwa joto kwenye titi. Dalili hizi huashiria kusambaa kwa saratani mwilini.

👉Dalili nyingine ni chuchu kutoa maji yasiyo ya kawaida ambayo hayana rangi. Aidha wakati mwingine, chuchu hutokwa damu au majimaji yenye rangi nyingine tofauti.

Ugunduzi wa Saratani ya Matiti
Pamoja na mgonjwa kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu na wataalamu wa afya kuweza kutambua uwepo wa tatizo hili, anaweza pia kufanyiwa vipimo vifuatavyo ili kusaidia kutambua ugonjwa huu.
X-ray ya matiti au Mammogram ambayo ina uwezo wa kuonesha ulipo uvimbe kwenye matiti
Ultra-Sonography ni kipimo kinachosaidia kutambua iwapo uvimbe uliopo ndani ya matiti umejaa maji ama la ili ufanyiwe vipimo zaidi
Kipimo kinachofanywa kwa kuchukua sehemu ya uvimbe (Aspiration) kwa kutumia aina fulani ya sindano (fine needle) na kisha kupeleka maabara sehemu iliyochukuliwa kwa ajili ya kutafitiwa zaidi ili kugundua uwepo wa saratani. Kwa kitabibu kipimo hiki hujulikana kama Fine Needle Aspiration and Cytology (FNAC)
Kipimo kingine ni upasuaji mdogo unaofanywa kwenye titi lililoathirika kwa ajili ya kuchukua sehemu ya titi (surgical biopsy) na kisha kuipeleka maabara kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Sentinal lymph node biopsy - Kipimo hiki hufanywa ili kujua kama saratani imesambaa hadi kwenye tezi.
Aidha kwa nchi zilizopiga hatua ya kimaendeleo, mgonjwa anaweza pia kufanyiwa vipimo kama

PET Scan: Hii ni aina mpya ya kipimo ambacho kinahusisha CT Scan na PET kwa pamoja. Kipimo hiki kina uwezo wa kutambua uwepo wa saratani ya matiti, iwapo saratani hiyo imesambaa ama bado, na kama itakuwa imeshasambaa, basi ni sehemu gani ya mwili iliyoathirika.
Aidha kipimo hiki, kina uwezo wa kutofautisha tezi au lymph nodes zilizovimba zina uhusiano na saratani (Metastatic lymph nodes) au hazina uhusiano na saratani (Benign lymph nodes).
Share:

WATCH OUT - MAHAFALI YA KIDATO CHA SITA BUSEGWE GIRLS HIGH SCHOOL 2020 - BUSEGWE SEC...

Hafla ya kuwaaga wahitimu wa kidato cha sita shule ya sekondari ya wasichana Busegwe yaliyofanyika kanisa la Waadventista Wasabato mtaa wa Busegwe sekondari - June 27, 2020
Share:

VERSE OF THE DAY - July 16, 2020


Let us therefore come boldly unto the throne of grace, that we may obtain mercy, and find grace to help in time of need.
Hebrews 4:16 KJV
Share:

VERSE OF THE DAY - July 14, 2020


Follow peace with all men, and holiness, without which no man shall see the Lord:
Hebrews 12:14 KJV
Share:

VERSE OF THE DAY - July 13, 2020


Jesus said unto him, Thou shalt love the Lord thy God with all thy heart, and with all thy soul, and with all thy mind. This is the first and great commandment. And the second is like unto it, Thou shalt love thy neighbour as thyself.
Matthew 22:37-39 KJV
Share:

HAPPY SABBATH - July 11, 2020


Share:

VERSE OF THE DAY - July 10, 2020


See that none render evil for evil unto any man; but ever follow that which is good, both among yourselves, and to all men.
1 Thessalonians 5:15 KJV
Share:

VERSE OF DAY - July 9, 2020


A new commandment I give unto you, That ye love one another; as I have loved you, that ye also love one another.
John 13:34 KJV
Share:

VERSE OF THE DAY - July 8, 2020


But thou, when thou prayest, enter into thy closet, and when thou hast shut thy door, pray to thy Father which is in secret; and thy Father which seeth in secret shall reward thee openly.
Matthew 6:6 KJV
Share:

VERSE OF THE DAY - July 7, 2020


But he was wounded for our transgressions, he was bruised for our iniquities: the chastisement of our peace was upon him; and with his stripes we are healed.
Isaiah 53:5 KJV
Share:

Translate

Categories

USOMAJI WA BIBLIA KWA MPANGO

...

BUSEGWE GIRLS HIGH SCHOOL

Tunapokea wanafunzi Kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 2021 kuanzia tarehe 7 Januari.
Pia nafasi za wahamiaji kidato cha tano zipo!
NYOTE MNAKARIBISHWA
Mawasiliano: +255759346439 (Mkuu wa Shule)
+255745114360 (Mhazini)

Support

Kanisa letu ni kanisa la shule ya sekondari ya wasichana Busegwe, katika jimbo la Mara. Shule hii ina uhitaji mkubwa wa kifedha kwa ajili ya maendeleo. Hivyo, kwa unyenyekevu, tunasihi sapoti yako ilikuweza kuiendeleza na kufanikisha programu mbalimbali ikiwemo uinjilisti.

Wasiliana nasi kwa mawasiliano yaliyo tolewa hapo chini au bofya HAPA