BUSEGWE GIRLS' HIGH SCHOOL

Tunapokea wanafunzi Kidato cha kwanza hadi cha nne kuanzia tarehe 7/1/2021 Pia nafasi za wahamiaji kidato cha tano zipo!
Mawasiliano: 0759346439 au 0745114360
NYOTE MNAKARIBISHWA

AFYA YETU - FAHAMU SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI (Cervical Cancer)

Saratani ya shingo ya kizazi (Cervical Cancer) ni saratani inayoanzia kwenye shingo ya kizazi (Cervix). Husababishwa na ukuaji usio wa kawaida wa seli ambazo zina uwezo wa kuvamia na kuenea sehemu mbalimbali za mwili.

DALILI: (SIGNS & SYMPTOMS)

  • Kutokwa na damu isiyo kawaida sehemu za siri (Ndani au nje ya mzunguko wa mwezi), 
  • Maumivu ya nyonga, 
  • Maumivu wakati wa tendo la ndoa na kutokwa damu baada ya tendo la ndoa

Pia virusi aina ya Human papillomavirus infection (HPV) huchangia asilimia 90 ya tatizo hili japokuwa si wote wenye virusi hivi hupata maambukizi hayo.

Sababu zingine za hatari ni pamoja na: 

  • Uvutaji wa sigara, 
  • Udhaifu wa kinga ya mwili (Immuno-comprimised patients)
  • Utumiaji wa vidonge vya uzazi wa mpango, 
  • Kuanza ngono katika umri mdogo
  • Kuwa na wapenzi wengi wa ngono.
  • Kujifungua (Ujauzito) zaidi ya mara saba

UTAMBUZI (DIAGNOSIS)

  • Kipimo cha picha (Medical imaging) hufanyika kutambua kiasi cha ueneaji wa saratani hiyo. 

KINGA (PREVENTION)

  • Chanjo aina ya HPV vaccines zinalinda dhidi ya aina mbili hadi saba za famililia ya HPV na kuweza kuzuia kiasi cha asilimia 90 ya maambukizi yake. 
  • Kama hatari za saratani bado zipo, miongozo inapendekeza kufanya vipimo vya  Pap tests.
  • Njia nyingine za kujikinga hujumuisha kutokuwa na wenzi wengi au kuacha kabisa. 
  • Tumia vyakula vya Vitamini (A, B12, C, E) na vyenye  beta-Carotene

MATIBABU

Inaweza kutibiwa kwa upasuaji, chemotherapy, na mionzi (radiation therapy).

Nb: Wahi kituo cha afya mara utapojiskia una dalili tajwa hapo juu.

 

Article by: Dr. Omar Ally +255746563122

 


Share:

No comments:

Post a Comment

Translate

Categories

USOMAJI WA BIBLIA KWA MPANGO

...

BUSEGWE GIRLS HIGH SCHOOL

Tunapokea wanafunzi Kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 2021 kuanzia tarehe 7 Januari.
Pia nafasi za wahamiaji kidato cha tano zipo!
NYOTE MNAKARIBISHWA
Mawasiliano: +255759346439 (Mkuu wa Shule)
+255745114360 (Mhazini)

Support

Kanisa letu ni kanisa la shule ya sekondari ya wasichana Busegwe, katika jimbo la Mara. Shule hii ina uhitaji mkubwa wa kifedha kwa ajili ya maendeleo. Hivyo, kwa unyenyekevu, tunasihi sapoti yako ilikuweza kuiendeleza na kufanikisha programu mbalimbali ikiwemo uinjilisti.

Wasiliana nasi kwa mawasiliano yaliyo tolewa hapo chini au bofya HAPA