-
Wahudumu wa Kambi la Busegwe 2020
Pr. PHILEMON MACHUGU(Mhutubu mkuu), Pr. CHARLES KITANITA, Pr. PAUL MALINDI Na Mwinjilisti PAUL OUMA. Kwa watoto walihudumiwa na Madam Consolata (Buhemba) na Maria Chacha(Mama Pasta Chacha)
-
Kanisa letu
BUSEGWE SECONDARY SDA CHURCH
-
Huduma za kanisa
Washiriki wakisikiliza Neno la Mungu
-
Huduma za uimbaji
MUHUBIRI ADVENTISTS CHOIR (Kwaya ya kanisa)
MATUKIO KATIKA PICHA: SABATO YA Trh19/12/2020 - Kumuaga Mwl DICKSON MKAMA (MHUBIRI ADVENTIST CHOIR)
SABATO TAKATIFU – JUMAMOSI 19/12/2020 - HUDUMA KUU
SOMO: USIKU UNAPOINGIA
MHUBIRI: Mwl. MKAMA DICKSON
FUNGU KUU: Kutoka
29:45-46
Mhubiri alianza na kisa alichopitia maishani mwake. Mnamo
mwaka 2019 akiwa jijini Dodoma
akifanya biashara zake miaka miwili baada ya kuoa, kwa bahati mbaya yeye na wenzeke kumi
walikamatwa na maofisa wa jeshi la polisi na kuwekwa rumande. Waliamriwa kutoa
kiasi cha Tsh. milioni moja kila mmoja ili kuachiwa huru ama kutumikia kifungo kisichopungua
miezi mitatu gerezani. Wakiwa rumande,
wenzake walifanya juhudi za kulipa faini hiyo ili waachiwe ila yeye hakufanya
jitihada hizo. Askari wale walimuuliza kwanini hafanyi harakati za kutoa kiasi
hicho, akajibu hana pesa hiyo, wakamwambia atabaki humo. Alijikabidhi mikonono
mwa Bwana Yesu kupitia maombi.
Ghafla! mke wake alianguka kwa mshituko wa moyo na kupoteza
fahamu kisha kupelekwa hospitali, ndipo
aliwaendea askari wale kuwaeleza namna ya kumsaidi ili ili aende
kumuuguza mkewe kwani hakuna ndugu wa karibu wa kumhudumia. Askari wale walimuuliza
kiasi cha pesa alichonacho ili wamuachie huru, akajibu kuwa ana kiasi cha Tsh
elfu 30 tu lakini kwa mashaka kwani nayo hakuwa nazo mfukoni(cash). Askari wale
walikataa kumkubalia lakini wakaenda
kujadili pembeni kisha wakamwita na kuweka mzigo wake kama dhamana kisha
wakamuachia.
Yohana 9:4
Yesu Kristo Anatukumbusha
kuwa kuna wakati wa kufanya kazi na upo
wakati tutapumzika kwani hatutaweza kufanya kazi hiyo. Yesu aliwaambia
wanafunzi wake juu ya kufanya kazi kwa
bidii kwani kuna wakati watakuwa wagonjwa ,katika umaskini,shida za
kifamilia,mfadhaiko au kufikia umri wa uzee ambapo watashindwa kufanya kazi
ipasavyo.
Katika kitabu cha Mhubiri, Suleiman anasema ukiwa kijana
unaweza kwenda popote pale na kwa mwendo wowote, lakini ukiwa mzee hutaweza
utapelekwa hata usikokutaka tena kwa mwendo usioutaka.Hivyo basi wakati tungali
na nguvu yafaa tumtegemee Mungu katika maisha yetu hasa wakati ambapo giza
linapoingia katika maisha yetu.
Tajiri mmoja katika mji Fulani aliyekuwa mfanyabiashara
maarufu katika mji ule,alikuwa na familia yake(mke wake na motto mmoja wa kike)Siku
moja asubuhi akiwa njiani kuelekea katika biashara zake akiwa katika gari lake
alipata ajali iliyotokana na tairi la mbele la gari yake kupasuka na gar
kupinduka.gari lake lilibondeka sana na raia walipo kuja kumsaidia baada ya
kumtoa akawa amevunjika mikono na miguu,hivyo wakampeleka hospitalin kwa
matibabu kasha akakaa kwa siku kadhaa akarudishwa nyumbani.baada ya siku chache
mke wake alipata mwaliko wa sherehe ya harusi ya mdogo wake baada ya kujadili
kama familia tajiri huyo alikubali mkewe aende kwa sherehe.Baada ya sherehe
kuisha walianza safari yeye na mwanae kurudi nyumban wakiwa njiani walikutana
na roli lililokuwa limepoteza mwelekeo kasha kugongana.Watu walipokuja kutoa
msaada walikuta mama huyo na binti yake wamepoteza maisha palepale,kumbe ni mke
wa Yule tajiri,n nani atapeleka taarifa kwa tajiri Yule kilema?kijana mmoja
akaamua kwenda,alipompa taarifa Yule tajiri aliinua macho yake juu kasha akasema
‘Bwana niko peke yangu kaa nami”
‘Kaa nami” ni
maneno yaliyotumiwa na Pr HENLY FRANCIS
aliyetunga wimbo no 91 katika nyimbo za
Kristo baada ya kukutana na changamoto katika maisha yake ikiwa ni pamoja na
ugonjwa na kukata tamaa, Aliita Bwana kaa nami. Bwana akikaa katika maisha yetu tutayashinda
yote yanayo tufedhehesha,.Mwite Bwana naye ataitika maana ameahidi.
MUNGU AWABARIKI NA
MUWE NA SABATO NJEMA.
NEW AUDIO: NINAYO HAJA - MHIBIRI ADVENTIST CHOIR
Unapoendelea kusikiliza wimbo huu tafakari ni jinsi gani amekuvusha na kukushindia changamoto mbalimbali. Barikiwa sana mtumishi katika Bwana.
Bwana aibariki MHUBIRI ADVENTIST CHOIR (Kwaya ya kanisa BUSEGWE SECONDARY SDA CHURCH)
AMEN.
VERSE OF THE DAY - 18th Dec 2020
1 Wathesalonike 5:16-18
16 Furahini siku zote;
17 ombeni bila kukoma;
18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
VERSE OF THE DAY - December 8, 2020
Warumi 15:4
Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini.
VERSE OF THE DAY - December 7, 2020
Marko 1:2-4
2 Kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya, Tazama, namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako.
3 Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
4 Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi
VERSE OF THE DAY - December 4, 2020
Isaya 43:2
Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.
Watch out - FORM FOUR Pre-GRADUATION 2020 - BUSEGWE GIRLS' HIGH SCHOOL
Kufungua Sabato na Pr. Endson Mabamba
Jumamosi - Shule ya Sabato & Huduma kuu
J'mosi jioni - Igizo kutoka kidato cha nne, Uimbaji, Sintosahau, Ushauri kutoka kwa watumishi, kufunga sabato
VERSE OF THE DAY - December 3, 2020
Waefeso 2:8-9
8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
VERSE OF THE DAY - December 2, 2020
Ephesians 2:8-9 KJV
For by grace are ye saved through faith; and that not of yourselves: it is the gift of God: Not of works, lest any man should boast.