HUDUMA KUU: EMMANUEL WANDIBA
SOMO: PAMBANO
FUNGU KUU: WAEFESO 6:11
Maandiko matakatifu yanatukumbusha juu ya habari ya uumbaji katika kitabu cha Mwanzo sura ya kwanza. Hapa utagundua ya kwamba Mungu aliumba dunia na vyote vilivyomo kwa namna ya ukamililifu na tena ya kuvutia, baada ya uasi (dhambi) pambano likaanza kati ya Mungu na shetani, wafuasi wa Kristo na shetani. Dunia ikageuka kuwa mahali pa mapambano.
Lakini Biblia inatukumbusha tuwe waaminifu katika kumtukuza Mungu ili tuzishinde vita dhidi ya muovu shetani. Yatupasa kufanya maombi ili kushinda Pambano hili.
Inawezekana miongoni mwetu tumekuwa na mazoea ya kwenda kanisani kutimiza ratiba na si kumtukuza Mungu. Hivyo yatupasa kuwa waaminifu katika ibada zetu ili kuimarisha Imani zetu kwa Mungu.
Lipo Pambano kubwa kati yetu ambalo pasipo uweza wa MUNGU hatuwezi shinda, na kujikuta tumekata tamaa.
Maandiko matakatifu yanatutia moyo kuwa endapo utaona unapambana vita ya kiroho, hata kukata tamaa lakini huoni ushindi, unapaswa uzidi kuwa imara na zaidi umtegemee MUNGU maana anakwenda kutushindia na kutenda miujiza dhidi ya pambano lako. Biblia inatuelekeza kuzivaa silaha zote za Mungu na tusikate tama kama anavyoeleza katika Biblia takatifu.
Yakobo 5:8
Yakobo anatutia moyo na kuwa na subira pindi tunapopambana kwani ni nyakati za mwisho kuja kwa Bwana Yesu Kristo na zaidi ya yote tunapaswa kushibisha mioyo yetu ili kuwa tayari kwa mapambano na ndipo tutahakikishiwa ushindi.
Mungu anatutaka tusimame imara na kuzivaa silaha zake dhidi ya hila za shetani ni hitaji langu mchana wa leo ya kwamba Mungu atutie nguvu katika kipindi hiki cha pambano ambapo sisi kama wafuasi wa kristo tunashambuliwa vikali , shetani amekuwa akianzisha vita kali dhidi yetu.
Mchana wa leo liwe hitaji lako ya kwamba Mungu azidi kutuimarisha zaidi ili tuweze kulikabili pambano lililo mbele yetu na mwisho atatushindia maana ametuhakikishia ushindi katika kila hatua tunayopitia.
BARIKIWA NA BWANA.
Amina
ReplyDelete