-
Wahudumu wa Kambi la Busegwe 2020
Pr. PHILEMON MACHUGU(Mhutubu mkuu), Pr. CHARLES KITANITA, Pr. PAUL MALINDI Na Mwinjilisti PAUL OUMA. Kwa watoto walihudumiwa na Madam Consolata (Buhemba) na Maria Chacha(Mama Pasta Chacha)
-
Kanisa letu
BUSEGWE SECONDARY SDA CHURCH
-
Huduma za kanisa
Washiriki wakisikiliza Neno la Mungu
-
Huduma za uimbaji
MUHUBIRI ADVENTISTS CHOIR (Kwaya ya kanisa)
VERSE OF THE DAY - June 30, 2020
VERSE OF THE DAY - June 21, 2020
VERSE OF THE DAY - June 19, 2020
VERSE OF THE DAY - June 18, 2020
VERSE OF THE DAY - June 17, 2020
KARAMA - MUHUBIRI CHOIR (Busegwe Sec SDA Church)
Tenor:- MASATU KAYORA & EMMANUEL WANDIBA
VERSE OF THE DAY - June 12, 2020
VERSE OF THE DAY - June 11, 2020
VERSE OF THE DAY - June 10. 2020
VERSE OF THE DAY - June 9, 2020
SAHANI YA MLO UNAOFAA
Healthy Eating Plate - Sahani ya Mlo Unaofaa
Sahani ya Mlo unaofaa, ambayo imebuniwa na wataalamu wa lishe kutoka Chuo Kikuu cha Afya ya Jamii, Harvard na kuhaririwa na wataalamu kutoka Harvard, ni muongozo wa mlo kamili unaofaa kwa afya-ikiwa utatumiwa kwenye sahani ya mlo ama kama chakula cha kufunga kwenye box. Bandika nakala kwenye fridge au kabati ili ikukumbushe kuandaa mlo kamili wenye afya!
- Sehemu kubwa ya mlo wako uwe mbogamboga na matunda – ½ ya sahani
Hakikisha unaweka aina mbalimbali zenye rangi tofauti. Viazi mbatata havihesabiwi kama mbogamboga katika Sahani ya Mlo unaofaaa kwa sababu ya madhara yake kwenye kiwango cha sukari mwilini.
- Tumia vyakula vya nafaka isiyokobolewa – ¼ ya sahani
Vyakula vinavyotokana na nafaka isiyokobolewa kama vile ulezi, mtama, mchele wa brown vinaathari kidogo katika kiwango cha sukari mwilini na utengenezaji wa insulini kuliko vyakula vinavyotokana na nafaka iliyokobolewa.
- Nguvu itokanayo na protini – ¼ ya sahani
Samaki, Kuku, maharagwe, njugu, vyote ni vyakula vinavyoleta afya kutokana na protini-vinaweza kuchanganywa na kachumbari, na pia kwenye Sahani ya Mlo Unaofaa vinafaa kuchanganywa na mbogamboga. Punguza matumizi ya nyama nyekundu and epuka nyama za kusindikwa kama beconi na soseji.
- Mafuta yatokanayo na mimea kwa kiasi
Chagua mafuta yanayofaa ambayo yanatokana na mimea kama vile mizeituni, soya, mahindi, alizeti, karanga na mengineyo na epuka kutumia mafuta ambayo yameganda. Kumbuka kuwa alama ya “low-fat” kwenye makopo ya mafuta haimaanishi “mafuta yafaayo kwa afya”
- Kunywa maji au chai
Epuka vinywaji vyenye sukari, punguza matumizi ya maziwa na vyakula vitokanavyo na maziwa mpaka mara moja au mbili kwa siku, punguza matumizi ya juisi mpaka glass ndogo moja kwa siku.
- Shughulisha mwili
Picha nyekundu ya mtu anayekimbia kwenye Sahani ya Mlo Unaofaa inakumbusha kuwa, kuweka mwili katika hali ya mazoezi ni muhimu pia katika kupunguza uzito.
Ujumbe muhimu wa Sahani ya Mlo Unaofaa ni kusisitiza kuhusu Aina ya Mlo unaofaa
- Aina ya wanga kwenye mlo ni muhimu zaidi kuliko kiwango cha wanga kwenye mlo, kwa sababu baadhi ya vyakula vya wanga mfano mbogamboga, matunda, nafaka zisizokobolewa na maharagwe vina manufaa kiafya kuliko zingine.
- Sahani ya Mlo unaofaa pia inashauri watumiaji kuepuka vinywaji vyenye sukari, ambavyo ni chanzo kikubwa cha kalori kwenye mwili, wakati vikiwa na faida ndogo kiafya.
- Sahani ya Mlo unaofaa inasisitiza utumiaji wa mafuta ya kupikia yatokanayo na mimea na haijamuwekea mtu kiwango cha juu cha asilimia ya kalori kutoka kwenye mafuta yanayofaa
NB: Coffee consumption is prohibited to all SDA members!
REFERENCE:
VERSE OF THE DAY - June 6, 2020
Juma la Kumi – Siku 100 za Maombi
“Kumlilia Yesu wakati wa uhitaji wetu mkuu!”
kukabiliana na dhoruba zijazo? Mambo yanapotokea ambayo yako nje ya uwezo wako, unageukia wapi kupata nguvu na faraja?
anakutumaini. Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele.” – Isaya 26:3-4
Paul Dysinger pamoja na mke wake Natasha wanaishi Tennessee wanapoendesha
Siku ya 71 – Kitovu cha Maombi – Ijumaa, 5 June 2020
Taarifa za Sifa!
• Alex G.: Mibaraka miwili mikubwa! Nilikuwa nimeanza kujifunza Biblia na daktari mmoja kutoka katika mji wangu. Na kwa sababu ya COVID-19 tumeweza kujifunza mara nyingi kuliko hapo awali. Alikubali kubatizwa hata kabla ya kuhudhuria kanisani! Mimi binafsi pia nilibarikiwa sana kwa kuwa hata kama ilibidi kuahirisha safari zangu mwaka huo, bado nilijipanga kwa namna iliyokuwa bora zaidi ili kupata nafasi ya kutosha kuomba, kusoma Biblia na kuandika huku nikifanya kazi kwa ufanisi zaidi. Katikati ya huzuni nyingi kulitokea pia mibaraka.
MAMBO YA KUOMBEA
1. Ombea ndugu na dada wanaopambana na ukosefu wa ajira wakati huu kwa sababu ya janga hili.
2. Tumwombee Magdalena na mume wake wanaoishi vijijini huko Columbia wakijaribu kuwafikia watu kwa ajili ya Yesu. Wanahitaji mahali pa kuabudia ili wawe wanakusanyika.
3. Omba kwa ajili ya makusanyiko yanayofanyika duniani kote ambao hawana mahali pa kuabudia wanapoweza kukutana kwa sababu ya hali iliyopo.
4. Ombea wale wanaojitolea kwa mwaka mmoja ambao wanasaidia wahamiaji wa Haiti kule Chile wanapojifunza lugha ya Kihispania na kujitahidi kuzoea maisha na utamaduni wa watu wa Chile. Mwombe Mungu afanye kazi kupitia kwa hao wanaojitolea, na kuwasaidia kujenga urafiki na Imani.
mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu,
nitampeleka kwenu.” – Mathayo 5:9
“Roho Mtakatifu alikuwa ndiye zawadi iliyo kuu ambayo Kristo aliweza kuomba kutoka
kwa Baba yake ili kuwainua watu wake. Ilikuwa Roho huyu atolewe kama kifaa cha
kuhuisha, na bila huyu kafara ya Kristo isingekuwa na maana. Dhambi ingeweza kukataliwa kupitia kwa uwezo mkuu wa wakala pekee aliye katika nafsi ya tatu ya Uungu
… Ni Roho ndiye anayewezesha matokeo bora ya kile kilichobuniwa na Mwokozi.
Maswali kwa Undani wa Moyo: Je, umewahi kukubali zawadi ya ajabu ya Roho Mtakatifu? Yeye ni sehemu ya Uungu, Mungu Baba, na Alitumwa kwako kama zawadi na Yesu. Anazungumza, anaongoza, anashawishi, anasaidia, anafariji, anabadilisha, na anakuwezesha katika mapito ya matengenezo na mabadiliko ili kuwa kama yeye aliye Yesu wetu mwenye upendo. Una Amani kumkaribisha Roho Mtakatifu katika maisha yako? Umepata uzoefu wake wa “kuwezesha matokeo bora ya kile kilichobuniwa na Mwokozi.” Kwa nini usikubali zawadi hii ya Roho Mtakatifu kutoka kwa Yesu na kumkaribisha moyoni mwako, ukimruhusu katika maeneo yote ya maisha yako?
TAARIFA ZA SIFA:
• Nicole P.: Nimeona watoto wangu wakikua katika urafiki na wenzao kadiri walivyocheza pamoja na kufanya kazi pamoja na marafiki zao. Tumekuwa na nyakati nzuri za asubuhi na jioni pamoja katika ibada za familia bila mmoja kukosa kwa sababu ya kazi au shule. Tumeshuhudia mambo mengi yakitendeka nyumbani mwetu, yote tukiyatenda pamoja. Na sasa tuna wingi wa maongezi ya kifamilia kuhusu matukio ya wakati wa mwisho.
• Gabriel A.: Ninamshukuru Mungu kwa uponyaji wake maalum katika kipindi hiki cha siku 100 za Maombi. Kiongozi wa nyimbo za Shule ya Sabato alitoa taarifa ya ugonjwa usiofahamika mguuni pake. Baada ya maombi, Mungu alimponya na akaendelea kuhudumu sabato iliyofuata, yaani Sabato ya tarehe 23 May 2020. Mungu Asifiwe!
MAMBO YA KUOMBEA
1. Ombea waumini kule Nigeria ambao wameathiriwa na mateso na uvamizi kutoka kwa makundi ya magaidi na hata kutoka kwa maofisa wa sehemu mahalia.
2. Omba kwa ajili ya mipango ya kujenga kituo cha mtindo wa maisha kule Puncak, Java Magharibi. Hapo ni muujiza unaohitajika!
3. Mwombee Martina R. ambaye amekuwa akipambana na ugonjwa wa kukosa kinga kwa miaka miwili sasa. Ugonjwa wake umemfanya ashindwe kushiriki katika kazi ya Mungu.
mioyo. Kwa hiyo anafunua makosa na kuyaondoa kutoka katika nafsi. Ni kwa
Roho huyo wa Kweli, akifanya kazi kupitia katika Neno la Mungu nidpo Kristo
TAARIFA ZA SIFA:
• Vasantha P.: Kwa sababu ya janga hili, nimepata muda wa kutosha wa kusoma Maandiko na kunukuu baadhi ya sehemu, nikitazama mahubiri na kusikiliza nyimbo za kiroho. Kufanya hivi kumenipatia nyakati tulivu za furaha kuliko nilivyowahi kuwa nazo!
• Carol D.: Ninamshukuru Mungu kwa neema yake na wema wake. Nimekuwa mshiriki wa kanisa la Waadventista wa Sabato kwa miaka 33, na janga hili limekuwa ni mbaraka kwangu, kwa sababu sikuwa nimetambua umuhimu wa matengenezo ya afya. Mungu amekuwa akifanya kazi moyoni mwangu.
Nimechagua kutumia vyakula vya aina ya mboga mboga. Mungu atukuzwe.
1. Omba kwa ajili ya makanisa ambayo yanapambana kuwezesha huduma zao kufanyika kidijitali kwa sababu wanakosa vifaa vya teknolojia hiyo pamoja na huduma za mtandao.
2. Ombea waumini wa Kiadventista wa Oman ambao wanajaribu kupata eneo la kukutania kwa ajili ya ibada baada ya janga hili.
3. Ombea familia ambazo zinapambana na adha ya kukandamizwa na nguvu za giza. Omba kwa ajili ya ushindi dhidi ya dhambi ambazo ni mlango wa kupitia wa Shetani anapokuja kuharibu.
4. Omba kwa ajili ya nyumba za Waadventista wa Sabato za wanawake wasiokuwa na makao kule Leipzig, Ujerumani. Huduma hii imesaidia kuhudumia wanawake takribani 2000 kwa zaidi ya miaka 25. Tafadhali mwombe Mungu aendelee kuwezesha huduma hii, kuleta matumaini, na uponyaji kwa wale wenye uhitaji mkubwa.
Siku ya 74 – Kitovu cha Maombi – Jumatatu 8 June 2020
Kristo anasema kwamba mvuto wa kimbingu wa Roho Mtakatifu utakuwa na
wafuasi wake hadi mwisho wa wakati. Toka siku za Pentekosti hadi yakati zetu hizi,
huyo Mfariji ametumwa kwa wote watakaojitoa kikamilifu kwa Bwana na kwa
huduma yake. Kwa hao wote watakaomkubali Kristo kama Mwokozi wao binafsi, huyo
Roho Mtakatifu atakuwa amekuja kwao kama mshauri, kiongozi, shahidi, na wa
Kristo kama mfano wetu leo hii; na katika Patakatifu pa Patakatifu tunakumbushwa umuhimu na uhalisia wa hukumu kadiri Kuhani Mkuu alivyoingia pale peke yake siku ya upatanisho (Yesu akishughulika katika hukumu ya upelelezi kwa niaba yako).
Kwa maneno mengine: Kazi ya Roho Mtakatifu ni kukuongoza katika uzoefu wa wokovu kupitia katika Imani kwa kila kitu ambacho Yesu amefanya na anaendelea kufanya kwa ajili yako. Unaweza kuona umuhimu wa uzuri wa kazi ya Roho Mtakatifu? Je, utakumbatia kazi yake ya kuhakikisha na kumruhusu siyo tu akuongoze kwa Yesu, bali pia akufanya ufanane naye kwa tabia katika matayarisho kwa ajili ya hukumu?
TAARIFA ZA SIFA:
• Makanisa mengi zaidi yameweza kuboresha majukwaa yao ya kidijitali na kuweza kufikia wengi wanaojihusisha na mitandao ya kijamii.
• John K.: Inashangaza kwamba wakati huu wa kutisha, waumini wa kanisa katika jimbo letu wamekuwa waaminifu katika kurejesha zaka na sadaka. Mwezi huu wa tano ulioisha tumevuka lengo letu la matoleo! Tunaomba asubuhi na jioni katika kipindi hiki cha siku 1 00 za Maombi. Na kwa kweli maombi haya siyo tu kwamba yamejenga hulka ya kushiriki katika maombi nyumbani, bali pia yameimarisha hulka hiyo. Usiku uliopita, watoto wangu wa kike wenye umri wa miaka miwili waliniita karibu kunapambazuka na kuniambia kuwa, “Baba, ni wakati wa maombi!” Ninamsifu Mungu nikitambua kuwa amepanda kile kilichokuwa kinapungua katika familia yangu – yaani hulka ya maombi.
1. Omba kwa ajili ya vijana na watu wazima, ambao wanapambana na uraibu wa mitandao ya kijamii
2. Ombea waumini kule Perth, Australia ambao wanaendelea kueneza injili kupitia katika barua kwa njia ya posta kwa jumuia yao.
3. Omba kwa ajili ya mtoto Tyson, kule New Zealand ambaye yuko katika uangalizi mkubwa wa kutegemeza uhai. Madaktari wanataka kuondoa mitambo ya kutegemeza uhai lakini tunaamini kwamba Mungu anafanya kazi pamoja na kwamba hajafumbua macho yake, wala kutoa sauti au kujongeza viungo vyake.
4. Ombea kituo cha maisha ya matumaini cha Waadventista wa Sabato kule Nazareth. Kituo hiki kinafundisha Kiingereza, Computer, madarasa ya afya na kadhalika. Mwombe Mungu abariki na kuendeleza huduma hii, kuwalinda na kuwaongoza wafanya kazi wanaojaribu kuifikia mioyo.
kutumikia wengine – utakua na kuzaa tunda. Neema ya Roho itakomaa katika tabia
yako. Imani yako itaongezeka, ushawishi wako utazama, upendo wako utakamilishwa.
Ndivyo utakavyoendelea kuakisi kufanana na Kristo katika yale yaliyo ya ukuu, yaliyo safi
na yenye upendo…. Tunda hili haliwezi kuharibika, bali litazaa mengine yanayofanana na
unaofanana na mti unaokua na hatimaye kutoa matunda. Lakini basi ni vyema kuwa na uhakika kwamba katika kujisalimisha na uaminifu, kila kipengele cha tunda la Roho kitakuwa dhahiri katika maisha yako!
Je, umemruhusu Roho Mtakatifu akuze ndani yako tunda lake? Kuna baadhi ya vipengele vya tunda la Roho ambavyo umekuwa ukimzuia asitende kwako? Ni haja yako kumuakisi Yesu zaidi na zaidi hadi watu wote waione tabia ya Yesu yenye upendo kwako?
TAARIFA ZA SIFA:
• Jones S.: Ninamshukuru Mungu kwa ajili ya siku hizi 1 00 za Maombi. Maombi haya yameleta nuru katika maisha yangu. Nimeanzisha mradi wa kuoka mikate wa Kiadventista katika kipindi hiki, na ninaeneza Neno la Mungu kupitia katika mradi huu wa kuoka mikate. Kupitia katika kazi ya Roho Mtakatifu, mmoja wa watu waliopata jumbe hizi ameamua kujiunga na kanisa la Waadventista wa
Sabato. Ninamshukuru Mungu kwa kunionesha njia nyingi tunazoweza kutumia kueneza Neno lake ili kuharakisha kuja kwake mara ya pili!
• Brother P.: Katika kipindi hiki cha kuzuiwa kutoka majumbani, nilipitia hatua ya kujiuliza maswali na kila juma, Mungu aliruhusu nipate majibu ya maswali yangu kupitia katika jumbe mbalimbali na uzoefu nilioshiriki na waandishi wa Siku 1 00 za Mombi. Ahsante sana Bwana kwa upendo wako mkuu na kwa nyakati za kushiriki ulizoruhusu tupate na dunia nzima.
MAMBO YA KUOMBEA
1 . Ombea wachungaji, wazee wa kanisa, na wahubiri walei duniani kote ambao wanajishughulisha na jitihada za uinjilisti kwa mtandao.
3. Omba kwa ajili ya kituo cha kusaidia waraibu wa pombe na madawa ya kulevya cha Waadventista wa Sabato katika mji mkuu wa Guatemala. Pamoja na kuwekwa huru kwa watu kutoka katika matumizi ya mihadarati, zaidi ya watu 1,500 wamebatizwa kwa huduma ya miaka tisa. Tafadhali mwombe Mungu aendelee kubariki, kuwezesha, na kubadilisha maisha ya wengi kwa ajili ya umilele.
4. Omba kwa ajili ya mgahawa wa Waadventista wa Sabato wa vyakula vya aina ya mboga mboga katika Byron Bay kule Australia. Mgahawa huo umeonekama kuwa nambari moja kwa umaarufu kama kijiwe cha watalii wa Kiaustralia. Omba kwamba Mungu abariki huduma hii na kwamba afanye kazi kupitia kwa mgahawa huu kufikia mioyo ya wengi.
Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?”
Luka 1 1 :1 3
walivyo tayari kuwapatia watoto wao zawadi zilizo nzuri. Kila mtenda kazi
kutii na kutenda mapenzi yake yaliyo mema, huku tukiwapenda wengine kama Yeye alivyotupenda. Ungeweza kumwomba Roho Mtakatifu kabla, lakini kwa kuelewa kwamba unahitaji ubatizo wake kila siku, je utaomba uwepo wake katika maisha yako? Utamkaribisha Roho Mtakatifu katika vyumba vyote vya moyo wako bila kuzuia chochote katika maisha yako?
TAARIFA ZA SIFA:
• Luis U.: Mimi na mke wangu tumekuwa tukitumia mtandao wa Skype katika kujifunza Biblia pamoja na watu wengine sita wakati huu wa kuzuiwa kutoka majumbani. Nimewakaribisha watu wengi kutazama program maalum inayorushwa na idhaa yetu ya Waadventista wa Sabato kule Brazil, na wengi ambao hata siyo Wakristo sasa wanafunguka kwa ujumbe wa Bwana wetu!
Baadhi ya rafiki zangu walio Wakristo wameanza kuamini katika kuja mara ya pili kwa Kristo!
• Winfrida M.: Ninataka kuwashirikisha neno la kutia moyo kwamba, maombi yanatenda kazi! Sabato iliyopita, watu watano walibatizwa kule Kinshasa baada ya program ya siku 1 00 za Maombi ambazo zilirushwa kupitia katika Radio, WhatsApp na mitandao mingine ya kijamii!
MAMBO YA KUOMBEA
1 . Omba kwa ajili ya waumini ambao wamerudi nyuma kwa sababu ya janga hili. Omba ili Roho Mtakatifu azungumze kwa uwazi katika mioyo yao. Omba kwa ajili ya wale wanaoweza kutoka na kuwafikia ili wapate ujasiri, hekima na upendo kadiri wanavyotafuta kuwasaidia ili warudi katika kutembea na Yesu kwa uaminifu.
2. Ombea waumini katika Konferensi ya Zimbabwe Mashariki ambao wanahangaika kutegemeza wenye uhitaji, wadhaifu, wazee, na wenye ulemavu katika jumuia yao.
Memorial Hospital Chattanooga, na hospitali zingine ulimwenguni kote.
Je, utatoa maisha yako leo kwa kazi ya kuongoa roho kwa ajili ya Yesu? Unatumainia kwamba Roho Mtakatifu atakuwezesha kufanya hata kazi inayoonekana kuwa haiwezekani? Utamwomba Yesu akubatize kwa roho kadiri unavyoingia na kuufikia ulimwengu unaokuzunguka?
• Mary F.: Kanisa letu limekuwa mbaraka mkubwa katika maombi ya kuunganika kipindi hiki cha siku 100 za Maombi. Kanisa linapata hisia ya uwepo wa Amani ya Mungu, nalo linaona mkono wake wenye nguvu.
• Ronald L.: Wakati huu wa kuzuiwa majumbani kikundi kidogo kilichokuwa na Waadventista wa Sabato wa zamani pamoja na watu wapya waliokuwa na shauku walishiriki katika kujifunza Biblia. Mimi kama mchungaji wao nilikutana nao, nikawaongoza katika huduma ya ibada ya uamsho. Mwisho wa mikutano tulipanga kuwa na huduma ya kuoshana miguu na meza ya Bwana. Kwa mshangao wetu, jumla ya waumini 52 walishiriki katika huduma hii, na asilimia 60 ya walioshiriki walikuwa ni waumini wa zamani ambao walimkubali Kristo na kufanya agano upya kupitia katika huduma hiyo ya meza ya Bwana. Napenda kumsifu Mungu kwa kujumuisha Papua New Guinea katika mpango wa siku 100 za Maombi siku ile ya 57. Mungu alijibu maombi yenu siku iliyofuata tarehe 23 mwezi wa tano kwa kurudisha kondoo wengi waliokuwa wamepotea katika kundi lake. Mungu asifiwe.
MAMBO YA KUOMBEA
1 . Ombea makanisa katika visiwa vya Caribbean ambayo pamoja na kushughulikia janga hili, sasa wanajitayarisha kwa ajili ya msimu wa vimbunga wa mwaka 2020.
2. Omba kwa ajili ya huduma ya kanisa la Waadventista wa Sabato la mji wa Ellicot, MD, Marekani kadiri wanaovyokusanya barakoa na glovu kwa ajili ya wafanyakazi wa idara ya matibabu.
3. Omba kwa ajili ya kanisa la vijana la Setagaya, ambao wanafanya kazi ya kujenga mahusiano na jamii inayowazunguka. Omba kwa ajli ya vijana na viongozi wao wapate kuona namna bunifu ya kutumikia mji wao.
4. Omba kwa ajili ya kituo vya mvuto cha maeneo ya mjini katika San Jose, kule Costa Rica, ambao wanaendesha madarasa ya mazoezi ya mziki, ushauri kwa familia, masomo ya Biblia na zaidi. Mwombe Mungu abariki jitihada zao za kuwafikia ili kuleta watu wenye uhitaji mkubwa wa kumfahamu.